Monday, May 21, 2012


Abdelbaset Ali al-Megrahi
Baadhi ya watu wanaamini al-Megrahi alishtakiwa kimakosa
Abdelbaset Ali al-Megrahi, ,tu wa pekee aliyeshtakiwa kwa kuilipua ndege kwa mabomu Lockerbie mwaka 1988, na wakati ambapo watu 270 waliuawa, amefariki baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.
Familia ya Abelbaset Ali al-Megrahi imeelezea kwamba hali yake ya afya ilizorota kwa haraka katika kipindi cha wiki chache zilizopita.
Dk Jim Swire, ambaye binti yake Flora ni kati ya waliokufa katika mlipuko wa Lockerbie, amesema kifo cha al-Megrahi ni habari za kusikitisha mno.
Anaanmini al-Megrahi alishtakiwa kwa makosa, na siye aliyehusika.
Bi Clare Connelly, ambaye ni mkurugenzi wa kikundi kinachojulikana kama Lockerbie Trial Briefing Unit katika chuo kikuu cha Glasgow, Uskochi, anasema wale wenye msimamo kwamba al-Megrahi alishtakiwa kimakosa, bado wameshikilia msimamo huo.
"Rambirambi nyingi zitatolewa kwa familia yake leo, baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. Na bila shaka masikitiko yataonyeshwa familia yake kwa kumpoteza na kwa mashaka waliyoyapata, lakini swali la mashtaka ya Lockerbie, na haki katika kumshitaki Bw Megrahi ni jambo ambalo bado halijatatuliwa", alielezea Bi Connelly.
"Kwa kumsikiliza Dk Swire, unapata hisia kwamba huenda mtu ambaye hakuhusika ndiye aliyeshtakiwa", aliongezea Bi Connelly.chanzo BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment