Mashabiki wa soka nchini
Rwanda wanaomboleza kifo mchezaji soka wa kimataifa kutoka nchini humo
Patrick Mafisango, mwenye umri wa miaka 32.
Mafisango, alikuwa amechaguliwa kuchezea kikosi
cha kitakachowania kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014
dhidi ya Algeria.
Alifariki katika ajali ya barabarani asubhi ya kuamkia leo mjini Dar es Salaam Tanzania.
Mchezaji huyo wa kiungo cha kati, anayechezea
kilabu ya Simba nchini Tanzania, ndio alikuwa amerejea tu kutoka Sudan
ambako timu yake ilishindwa katika michuano ya kuwania kombe la
Confederation mwsihoni mwa wiki.
Kocha wa kilabu hiyo ameelezea kuhuzunishwa sana na tukio hilo.
Mafisango alifariki katika ajali iliyohusisha
pikipiki na gari wakati gari alipokuwa anaenesha lilipoteza mwelekeo na
kuanguka kwenye mtaro.
Alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi msimu huu
wa mechi za ligi ya Tanzania kwa kuingiza magoli, 12 na aliitwa na kocha
Sredrojevic kushiriki mechi ya kufuzu kwa michauano ya kombe la dunia
itakayofanyika mwezi ujao.
CHANZO CHA HABARI KUTOKA http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo/2012/05/120517_mafisango_aaga.shtml
0 comments:
Post a Comment