KESI ya msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ (17), jana
ilipigwa kalenda hadi Juni 11 mwaka huu kwa ajili ya maombi yake
kuhusiana na uhalali wa umri wake yatakapotolewa uamuzi.
Jaji wa Mahakama Kuu, Dk. Fauz Twaib, anayesikiliza shauri hilo,
alisema kutokana na utetezi kuwa mrefu, hana budi kupata muda ili aweze
kuupitia na kuutolea uamuzi Juni 11 katika mahakama hiyo.
Mawakili wanne, Jacqueline Dimelo, Kennedy Fungamtama, Fulgency
Massawe na Michael Kibatala ambao wanamtetea Lulu, wameiomba Mahakama
hiyo kuchunguza umri wa Lulu au watoe idhini kwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kufanya hivyo.
Hata hivyo, hali ilikuwa ya utulivu mahakamani hapo, tofauti na
ilivyozoeleka mwanzoni mwa kesi hiyo ilivyoanza kusikilizwa, ambako pia
mtuhumiwa alikuwa katika hali ya kawaida na kuwa na sura yenye tabasamu
na kuweza kupeana ishara ya salamu na baba yake mzazi aliyefika kusiliza
kesi ya binti yake.
Mara kwa mara, Lulu alikuwa akipepesa macho kila kona ndani ya
mahakama hiyo na hata kuwaangalia watu wachache waliokuwemo ndani.
Mawakili wa Lulu, wanadai mteja wao ana miaka chini ya 18 hivyo shauri lake linapaswa kuendeshwa katika mahakama ya watoto.
Lulu anakabiliwa na tuhuma za kusababisha kifo cha aliyekuwa msanii
mwenzake nyota wa filamu hapa nchini, Steven Kanumba, aliyefariki Aprili
7 mwaka huu nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI : Tanzania Daima http://www.freemedia.co.tz
CHANZO CHA HABARI : Tanzania Daima http://www.freemedia.co.tz
0 comments:
Post a Comment