Wasanii wanaijua ile hamu kubwa ya kuwa superstar ama
celebrity wakati wanaporekodi single yao ya kwanza na kuipeleka redioni.
“Bonge
la track mwana” ni sentensi yenye maneno manne tu lakini inayoweza kumfanya
underground alale usingizi mnono siku hiyo.
Mambo huanza kubadilika taratibu pale airplay za kutosha
zinapokuwepo kwa ngoma ya underground huyu.
Baada ya miezi michache, simu yake
inaanza kuwa busy kwa simu kutoka kwa watangazaji wanaotaka interview,
mapromoter wanaotaka kufanya naye show na mashabiki wanaotaka kumpa big up tu.
Tayari ameshakipata alichokuwa akiitoa kwa muda mrefu “usupastaa”.
Maisha yanabadilika na kero zinakuwa nyingi.Msanii anapokuwa kwenye stage hiyo hawezi kuepuka kusemwa
vibaya.
Kwa Lady Jaydee lakini usumbufu huu umeanza kumkuta kitambo sana. Ni
wazi kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wa Bongo wanaosemwa zaidi.
Kuanzia
uhusiano wake na Gadner mpaka suala la kutokuwa na mtoto hadi leo hii.
Hapa katikati magazeti ya ‘umbea’ yalikuwa yamempa likizo
kidogo. Lakini kwa ujumbe huu hapa chini ulioandikwa na yeye mwenyewe, bila
shaka pua za wadaku zishaanza kunusanusa pande zake kutafuta story ya kuuzia
gazeti.
0 comments:
Post a Comment