RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameteua wakurugenzi wapya tisa wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na
hadhi ya balozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es
Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo
umeanza Mei 2, mwaka huu.
Walioteuliwa ni Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya
Afrika; Naimi Aziz (Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda);
Celestine Mushy (Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa); Yahya
Simba (Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati), na Bertha Somi ambaye
ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.
Wengine ni Irene Kasyanju (Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria); Dorah
Msechu (Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika); Mbelwa Kairuki
(Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia) na Silima Haji ambaye
ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, Kibwana alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu; Naimi
Aziz (Mkurugenzi Msaidizi), Mushy (Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu), Simba (Afisa Mambo ya Nje Mkuu), na Somi alikuwa Afisa
Mambo ya Nje Mkuu.
Wengine; Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Msechu (Mkurugenzi
Msaidizi), Kairuki (Msaidizi wa Rais - Hotuba, Ofisi ya Rais, Ikulu) na
Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.
CHANZO CHA HABARI: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment