Wednesday, May 16, 2012

Hoteli moja maarufu visiwani Mombasa imeshambuliwa kwa maguruneti na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Magaidi washambulia hoteli kando ya mahali hapa
Hoteli hiyo ,Bella Vista Restaurant,ni maarufu sana kwa watalii na wenyeji na iko kando ya barabara kuu itokayo bandari ya Mombasa.
Mkuu wa kitengo cha polisi wa jinai mjini Mombasa Bwana Ambrose Munyasya aliambia BBC kuwa watu watano walijeruhiwa vibaya katika kisa hicho.
Polisi wanasema kuwa uchunguzi wao wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na milipuko mitatu katika klabu hicho cha Bella Vista Restaurant.
Milipuko hiyo ilisababisha uharibifu wa magari sita yaliokuwa yameegeshwa kando ya hoteli hiyo.
Mkuu huyo wa polisi alisema kufikia sasa wanahofia kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na magaidi.
Inadaiwa kuwa watu wawili walikwenda katika Klabu hicho wakitaka kuruhusiwa kuingia.
Lakini walipotakiwa kupekeliwa na maaskari wa hoteli hiyo walikataa na ndipo wakarusha maguruneti hayo.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa magaidi hao walifyatua risasi ovyo ovyo wakati walipokuwa wakitoroka.
Hata hivyo polisi wanasema hawaja mkamata mtu yeyote kutokana na kisa hicho.

0 comments:

Post a Comment