Beki kisiki wa zamani wa wa Manchester United, Jaap Stam amesema hana urafiki na kocha wake wa zamani, Alex Ferguson.
Lakini
Stam raia wa Uholanzi akasisitiza, hana matatizo wala kinyongo na
Ferguson ingawa uondoka yake katika klabu haikuwa ya kiungwana.
“Wakati
huo sikufurahia, haikuwa vizuri namna alivyoniondoa. Lakini yale
yamepita na sasa sina tatizo naye,” alisema Stam aliyekuwa mmoja wa
mabeki maarufu wa kati duniani wakati akiichezea Man United na baadaye
AC Milan.
Stam
sasa ana umri wa miaka 43, alikataa kwenda Liverpool na kujiunga na Man
United ambayo alifanikiwa kubeba ubingwa wa England mara tatu ukiwemo
ule ushindi wa kihistoria wa mwaka 1999 wakati Man United ilipobeba
ubingwa wa England, Ligi ya Mabingwa Ulaya na ubingwa wa Dunia.
0 comments:
Post a Comment