Friday, October 25, 2013

Mahojiano ya mwandishi wa jarida la biashara na uchumi, John Stephen na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapatao Tanzania (TRA), Harry Kitilya yamechapishwa kwenye gazeti la Mwananchi kuhusu mamlaka hiyo nyeti ya Serikali inayosaidia kuandaa bajeti ya serikali kwa manufaa ya Watanzania wote.

Moja ya maswali aliyoulizwa ni je: Ni lini wamiliki wa nyumba binafsi za kupanga watalipa kodi? ambalo Kitilya alijibu:
Kwa mujibu wa kifungu namba 86 cha sheria hiyo, mapato ya upangishaji wa nyumba yanayozidi Sh500,000 kwa mwaka, ndiyo yanayotozwa kodi ya mapato. Mapato chini ya kiwango hicho hayatozwi kodi, na mpangishaji mwenye mapato hayo
hulazimika kisheria kujisajili au kusajiliwa kama mlipa kodi. Kwa mfano, nyumba yenye vyumba vinne ambavyo vinapangishwa kwa Sh10,000 kila kimoja kwa mwezi, mapato yake ni Sh480,000 kwa mwaka.

Mapato hayo hayatozwi kodi kwa vile yapo chini ya Sh500, 000. Mapato zaidi ya hayo yanatakiwa kulipiwa kodi kwa utaratibu wa zuio (Withholding Tax) na mpangaji ndiye anayetakiwa kumkata mpangishaji kodi hiyo wakati anapofanya malipo na kuwasilisha makato TRA, kama mpangaji huyo siyo mtu binafsi. Iwapo mpangaji ni mtu binafsi, wajibu wa kulipa kodi ni wa mpangishaji.
  • Lini mtaanza kutoza kodi ya ardhi, mashamba, nyumba, kama nchi nyingine zinavyofanya?
  • Ni nini msimamo wa TRA kuhusu biashara, zinazofanyika nchini kama vile za kupangisha majengo ya biashara, ofisi Dar, Mwanza, Arusha na kwingineko ambazo malipo yake yamekuwa yakifanyika kwa US dollar badala ya shilingi?
  • Malipo yakifanyika kwa US dollar yana athari gani kiuchumi hasa kwa jamii?
  • Wanaolipa kodi wangependa kujua, hivi sasa mnakusanya shilingi ngapi kwa mwezi?

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/10/wamiliki-nyumba-za-kupanga-wanalipa-kodi-mapato-yakizidi-shilingi-ngapi.html#ixzz2ihTYddbT

0 comments:

Post a Comment