Thursday, August 15, 2013

Wakati sakata la kodi ya simu ya Sh1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayotakiwa kulipwa na watumiaji wa simu likiwa limerejeshwa bungeni na Serikali, Spika wa Bunge, Anne Makinda ameibuka na kusema fedha hiyo ni ndogo na kila Mtanzania ataweza kuilipa.

Spika Makinda alishangazwa na Mtanzania anayeshindwa kupata Sh1,000/= kwa mwezi, kufafanua kuwa kama wananchi wataifanya nchi yao kuwa rahisi, watalalamika na umaskini mpaka siku watakayokufa. ...

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Bajeti, Spika Makinda alisema, “Haya maendeleo tunayoyataka sisi kama Watanzania yatapatikana kwa kulipa kodi, hata vitabu vitakatifu vinasema kila mtu lazima achangie. Bila kukusanya kodi nchi itashindwa kujiendesha na kusisitiza kuwa kama angeulizwa kuhusu masuala ya ulipaji kodi angesema uanzishwe hata mfuko maalumu wa kuwasaidia vijana.”

Alisema kwa kuwa suala hilo la kodi hivi sasa ni sheria, mabadiliko yake ni lazima yarudi bungeni na akasisitiza kwamba hata hivyo haamini katika kushindwa kulipa fedha hiyo.

“Tunataka kufanya vitu vingi na hatuwezi kuitegemea Serikali katika kila kitu sasa yenyewe itatoa wapi fedha. Hayo ni maoni yangu lakini hiyo ni sheria,” alisisitiza Spika Makinda.

0 comments:

Post a Comment