Tamko hili limetolewa leo tarehe 3 august 2013, mkoani mbeya
katika ukumbi wa royal zambezi
KIKAO CHA WALIMU WA MKOA WA MBEYA CHA KUJADILI MASLAHI YA WALIMU WA
TANZANIA-Tarehe 3 August, 2013.
1.
CHAMA
CHA WALIMU-CWT NA WALIMU.
a. Umuhimu
wa chama cha walimu katika kufuatilia maslahi na madai mbalimbali ya walimu.
CWT imeshindwa kuwasaidia walimu katika kufuatilia madai ya maslahi mbalimbali
kama vile kupanda madaraja, malimbikizo ya mishahara, nauli n.k ambapo jukumu
la chama sasa jukumu hili limekuwa likifanywa na walimu wenyewe alihali
tukichangia chama kwa ajili ya kutetea walimu.
b. Uwajibikaji wa Chama
cha walimu-CWT kwa walimu. CWT imeshindwa:-
i.
Kutoa, elimu, taarifa, mbalimbali kwa walimu hii ikiwemo katiba ya Chama
Cha Walimu-CWT, Kanuni za kudumu utumishi wa umma kwa walimu ili
kutufanya tutambue vizuri haki na wajibu wetu kama watumishi.
ii.
Kutoa taarifa kwa walimu juu ya mwenendo wa majadiliano kati ya serikali
na CWT kuhusu madai ya nyongeza ya mishahara kwa 100%, posho ya mazingira
magumu, posho ya kufundishia na posho ya walimu wa sayansi n.k. CWT imekaa
kimya kwa muda sasa tangu mahakama isitishe mgomo wetu na kutuamuru turudi
kazini huku mahakama ikiiamuru serikali kukaa meza moja na CWT ili kufikia
muafaka. Umepita muda sasa chama cha Walimu-CWT hakijatoa taarifa yoyote kwa
walimu kuhusu hatma ya madai hayo ya walimu. Hii inadhihirisha kuwa chama cha
walimu aidha kimeamua kuwasaliti walimu kwa kushirikiana na serikali yaani
mwajiri wetu.
c. MCHANGO
wa kila mwezi. Walimu wa mkoa wa Mbeya kwa niaba ya walimu wa Tanzania tunahoji
uhalali wa chama cha walimu-CWT kukata fedha kila mwezi kama mchango wa chama
alihali si wanachama wa Chama hicho.
2. SERIKALI YA JAMHURI
MUUNGANO WA TANZANIA NA WALIMU
Serikali ya jamhuri ya muungano
wa Tanzania imekuwa ikifanya yafuatayo kwa kwa kada ya utumishi wa umma hasa
ualimu:-
a. Kuligawa
Taifa kimakundi na kuvunja umoja wa kitaifa kwa kufanya yafuatayo:-
i.
Kuweka tofauti kubwa ya kipato cha mshahara kwa wafanyakazi wa serikali
wenye elimu sawa katika kada tofauti. Mfano kwa mujibu wa waraka wa watumishi
wa serikali Na 1. Wa mwaka 2013, wenye Kumb. Na. CAC.205/228/01/C/14
wa Julai 2, 2013 uliosainiwa na Katibu mkuu Utumishi Ndugu George D. Yambeshi.
Unaoonyesha marekebisho ya mishahara kwa watumishi wa serikali. Katika waraka
huu unaendelea kudidimiza kada ya ualimu kulingana na kada zingine kama vile
kada ya afya, sheria na kilimo na utafiti ambapo kada hizi hulipwa mishahara
mikubwa kuliko ya walimu. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2005 ibara ya 23(1) inasema “Kila
Mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira
unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao
watapata malipo kulingana na uwezo na kiasi kiasi na sifa za kazi
wanazozifanya”. Je, serikali ya Jamhuri ya Muungano inatulipa walimu
ikitofautisha mshahara huo na kada zingine kwa vigezo kwamba:-
a. Uwezo
wetu wa kufanya ya kazi haufanani na kada hizo?
b. Umuhimu
wa kada ya ualimu ni mdogo tofauti na kada hizo nyingine?
c. Sifa
za kielimu walizonazo walimu ni tofauti kabisa na kada hizo?
d. Umuhimu
wa walimu na elimu ni mdogo katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania
ukilinganisha na sekta kama vile Kilimo na Afya?
e. Au
hii ni mbinu ya “divide and rule” kwa wafanyakazi?
NGAZI YA
ELIMU
|
UALIMU/ ELIMU
|
KILIMO
|
AFYA
|
Certificate (Cheti)
|
Tsh 344,000/=
|
Tsh 1,060,000/=
|
Tsh 562,000/=
|
Diploma
(Stashahada)
|
Tsh 432,500/=
|
Tsh 1,252,000/=
|
Tsh 821,000/=
|
Degree (Shahada)
|
Tsh 589,000/=
|
Tsh 1,473,000/=
|
Tsh 994,000/=
|
Jedwali hili ni kwa
mujibu wa waraka huo uliotajwa hapo juu
|
b. Kulubuni
vyama vya wafanyakazi ikiwemo Chama cha Walimu-CWT ili kuacha majukumu yake ya
kutetea na kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa wafanyakazi ila vyama hivyo
kushirikiana na serikali kukandamiza haki za wafanyakazi. Baadhi ya mbinu
ambazo serikali imekuwa ikizitumia ni kama vile:- Moja, kuwapatia posho kubwa
wakilishi na viongozi wa vyama pindi serikali na wawakilishi hawa wanapo kutana
katika kujadili maslahi ya wafanyakazi ili kuwaziba mdomo. Pili, Kuwatishia
kusitisha utaratibu wa kukusanya michango ya wanachama ila vyama vyenyewe
vikusanye kwa njia wanaoijua wao. Tatu, kutofanya ukaguzi wa mara kwa mara
katika vyama hivi vya wafanyakazi katika mapato, matumizi na miradi mbalimbali.
Hii inasababisha vyama vya wafanyakazi kutofanya kazi ya kutetea wafanyakazi
bali kutumia fedha na mali za vyama kwa manufaa binafsi.
c. Kutumia
vitisho na kauli za kutisha kudidimiza maslahi na haki za watumishi wa umma
ikiwemo walimu. Viongozi wa serikali kama mawaziri na viongozi wengine
waandamizi wa serikali wamekuwa wakitumia vitisho kwa wafanyakazi kama njia ya
kuwanyamazisha wasidai maslahi yao.
3.
TAMKO
KWA CHAMA CHA WALIMU-CWT NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Sisi Walimu wa Mkoa wa Mbeya tunatoa siku 30 kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na Chama Cha Walimu-CWT, Kuanzia leo Tarehe 03
August, 2013 hadi Tarehe 03 September, 2013 itekeleze yafuatayo:-
I.
CHAMA
CHA WALIMU-CWT
· Kutoa taarifa
ya fedha ya (Makusanyo ya kila mwezi) na mapato na matumizi ya chama hicho kwa
walimu.
· Kutoa taarifa
ya wapi wamefikia kuhusu madai yetu dhidi ya serikali ya nyongeza ya mishahara
kwa 100% na posho za mazingira magumu na kufundishia n.k, kwani ni muda sasa
walimu tumechoka na ukimya wa CWT juu ya suala hilo.
· Chama
kisitishe makato haraka kwa walimu ambao si wanachama wa chama hicho.
· Mkaguzi mkuu
wa serikali (CAG) akague mwenendo wa miradi, mapato na matumizi ya Chama Cha
Walimu-CWT na kutoa Taarifa kwa Walimu.
· Kuboresha
mfumo wa mawasiliano kutoka viongozi wajuu wa chama hadi walimu katika ngazi ya
tawi.
II.
SERIKALI
YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
· Serikali iweke
sawa uwiano wa mishahara kisekta kulingana na viwango vya elimu kwa watumishi
wa umma.
· Serikali
isitishe vitisho na matamko yenye vitisho kwa watumishi wa umma.
· Serikali
ipunguze kiwango cha kodi kubwa na kandamizi kwa watumishi wa umma, na itafute
vyanzo vingine vya mapato
· Serikali
isizue watumishi kujiendeleza kwa sababu yoyote ile ili mradi wawewamekidhi
vigezo vya kisheria vya kujiendeleza.
· Serikali
isitishe mpango wa kuligawa taifa kwa misingi ya maslahi binafsi, Kielimu,
Kisekta na Nyadhifa.
· Serikali
ipandishe madaraja walimu waliojiendeleza kielimu ili kuwapa motisha.
Imetolewa na Walimu Wa Mkoa Wa
Mbeya-Tarehe 03 August, 2013- Mkoani Mbeya.
0 comments:
Post a Comment