Mpango
wa Matokeo Makubwa Sasa (Elimu) ulizinduliwa na Waziri wa Elimu na
Mafunzo jana na kutaja mikakati 9 ifuatayo: Hebu pitia mikakati
hii-kisha utoe maoni yako kama inajitosheleza.
1. Upangaji wa
shule kwa ubora wa matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule iliyoongoza
hadi ya mwisho. Lengo la mkakati huu ni kuongeza uwajibikaji na ushiriki
wa jamii katika usimamizi wa utoaji wa elimu bora....
2.
Utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. Utaratibu wa kutoa tuzo kwa
shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora
zaidi.
3. Kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule. Mkakati huu
utasaidia kuimarisha utendaji wa shule kwa kuwawezesha viongozi wa shule
kutekeleza majukumu yao kikamilifu
4. Upimaji wa kitaifa wa
stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu. Lengo la mkakati huu ni kuhakikisha
wanafunzi wanamudu stadi msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu katika
madarasa ya chini ya elimu ya msingi kabla ya kujiunga na madarasa
yanayofuata
5. Utoaji mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji
mahiri wa stadi za KKK. Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha walimu
kumudu ufundishaji wa stadi za KKK katika darasa la kwanza na la pili.
Mafunzo yatatolewa kwa walimu kutoka shule 6,167 za halmashauri 40.
6. Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji
na kujifunza-Students Teachers Enrichment Program (STEP). Mkakati huu
utajenga utamaduni wa kuwabaini wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika
kujifunza. Aidha, utoaji mafunzo ya walimu kwa ajili ya utekelezaji
yanalenga kumpa mwalimu nyenzo na uwezo zaidi wa kufundisha na kubaini
na kuzingatia maeneo yenye changamoto kwa wanafunzi.
7. Ujenzi
wa miundombinu muhimu ya shule. Lengo la mkakati huu ni kuboresha
mazingira ya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa vifaa muhimu
shuleni.
8. Utoaji ruzuku ya uendeshaji wa shule. Utekelezaji
wa mkakati huu utawezesha uboreshaji wa upatikanaji vitabu vya kiada na
vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
9. Utoaji wa
motisha kwa walimu. Mkakati huu utawezesha kuwatambua walimu, kutatua
changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha za kifedha na zisizo za
kifedha kwa kujali maslahi na madai yao ya kimsingi.
0 comments:
Post a Comment