Dar es Salaam.
Ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya 37 ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (TanTrade), umesogezwa mbele kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama.
Ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya 37 ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (TanTrade), umesogezwa mbele kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama.
Maleko alisema kutokana na hali hiyo, maonyesho hayo hayatafunguliwa siku hiyo, hadi wageni hao watakapoondoka nchini.
Alisema huenda yakafunguliwa kuanzia Julai 4 au 5, kulingana na ratiba itakayotolewa na Serikali.
“Ilikuwa tuzindue rasmi Julai Mosi, lakini
tumebadilisha kutokana na ugeni wa viongozi hao, jambo ambalo mpaka sasa
Serikali haijatoa taarifa rasmi ya tarehe maalumu ya ufunguzi huo,”
alisema Maleko.
Maleko alisema kulingana na ratiba iliyopo, maonyesho hayo yatafunguliwa kama kawaida Juni 28, mwaka huu hadi Julai 8, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi.
Alisema kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara wa
ndani wanaweza kujenga mtandao wa biashara na wenzao wa nje, hiyo
itawasaidia kupata masoko na kuongeza uzoefu.
Maleko alisema maonyesho ya mwaka huu, kutakuwa na bidhaa maalumu za ndani zitakazoonyeshwa kwa siku tofauti; asali, korosho na sanaa ya uchongaji.
Alisema lengo ni kutangaza soko la uzalishaji
bidhaa hizo, jambo ambalo linaweza kuongeza masoko na kukuza mitaji kwa
wazalishaji.
Pia, katika siku hizo, kutakuwa na siku maalumu ya kutangaza nembo ya Tanzania (Tanzania Brand) ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa sababu ndiyo muasisi wa siku nembo hiyo.Alisema tiketi za kuingilia kwenye maonyesho hayo zitaanza kuuzwa Juni 26.
0 comments:
Post a Comment