Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Luaha Kilosa
Mkoani Morogoro wakati yeye akiongozana na baadhi ya wajumbe wa
Sekretarieti ya CCM wakati katibu mkuu huyo alipofanya ziara katika
eneo hilo, Katibu mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi ya kuhimiza
maendeleo na kukagua miradi ya maendeleo ili kuisimamia serikali katika
kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwahamasiha wananchi katika
kushiriki shughuli za maendeleo.
Katibu mkuu huyo ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ruaha wilayani Kilosa ikiwa ni mkutano wake wa kwanza mara baada ya kuanza ziara yake ya siku saba mkoani Morogoro kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
Kinana amesema kuwa hoja zinazotolewa na wapinzani lazima zipimwe na kufanyiwa kazi badala ya kubezwa, akisisitiza kuwa tabia ya kubeza kila hoja ya wapinzani imechangia viongozi wengi kushindwa kuwajibika kwa wananchi.
Baada ya kuwahutubiwa wananchi katibu mkuu huyo akatoa nafasi kwa wananchi kuelezea kero zao na akalazimika kujibu baadhi ya hoja hizo ambapo kwa upande wa kero za wakulima wa miwa amehadi kufikisha tatizo hilo kwenye kamati kuu ya CCM, CC .
Awali katibu mwenezi wa CCM taifa Nape Moses Nauye katika utangulizi wake amewapongeza wananchi kwa ushiriki wao katika kutoa maoni ya katiba na uundwaji wa mabaraza ya katiba
Praxeda Mtani, TBC Morogoro.
0 comments:
Post a Comment