KUZALIWA;
Mhe. Salimu Hemed Khamis(Marehemu)
alizaliwa shehia ya Mizingani jimbo la Chambani tarehe 20 Septemba 1951 .
ELIMU YA MSINGI;
• Mwaka 1959-1960 alisoma katika shule
ya msingi Pandani.
• Mwaka 1960 – 1967 alisoma katika shule ya
msingi Kengeja na kuhitimu elimu ya msingi.
ELIMU YA
SEKONDARI;
• Marehemu alijiunga na masomo ya sekondari mwaka 1968
katika shule ya Sekondari ya Chambani iliyoko Pemba na alisoma hapo hadi
mwaka 1969.
• Ilipotimu mwaka 1970 marehemu aliendelea na masomo
ya sekondari katika shule ya sekondari ya Fidel Castro na alihitimu
mwaka 1971.
• Mwaka 1972 marehemu alijiunga Lumumba Sekondari,
zamani ikiitwa “LUMUMBA COLLEGE” kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano
sita na alihitimu mwaka 1973.
ELIMU YA JUU;
• Marehemu
alisomea shahada ya kwanza Bachelor of Science in Agronomy 1978 -1982
huko Havanna nchini Cuba.
• Mwaka 1988 – 1989 alijiunga na chuo cha
Commonwealth Mycological Institute kilichoko nchini Uingereza (UK) na
kusomea shahada ya uzamili ya masuala ya “Plant Disease Management”
yaani “utaalamu wa magonjwa ya mimea”
MAFUNZO YA KITAALAMU;
• Mwaka 1987 - Marehemu alishiriki na kuhitimu mafunzo ya uongozi ya
“SENIOR MANAGEMENT COURSE ON AGRICULTURE” huko nchini Uswisi.
•
Mwaka 1989 - Marehemu alishiriki mafunzo maalum ya “UTAFITI WA
VIRUTUBISHI WA MIMEA” yaani “IDENTIFICATION OF PATHOGENIC FUNGI AND
BACTERIA” katika chuo cha “Commonwealth Mycological Institute” CMI huko
LONDON - Uingereza,
UTUMISHI WA UMMA;
Marehemu ametoa
mchango mkubwa katika sekta ya umma kwa upande wa Zanzibar na Tanzania
Bara kutoka na elimu kubwa na adimu aliyojaliwa na mwenyezi mungu
sambamba na ujuzi;
• Marehemu alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari
Mtambile Pemba chini ya wizara ya elimu mwaka 1974 – 1978.
• Mwaka
1977 – 1978 alifundisha pia katika Shule ya Sekondari Fidel Castro –
Pemba.
Katika kusukuma gurudumu la kilimo ambalo ndilo uti wa
mgongo wa taifa, marehemu alitumia ipasavyo utaalam na ujuzi wake wa
hali ya juu wa masuala ya usimamizi wa mimea kwa kusimamia mashamba
kadhaa ya kilimo;
• Mwaka 1984 - 1996 alikuwa meneja wa shamba la
Shirika la Sukari na Manukato la Mahonda lililoko Zanzibar.
• Mwaka
1997 hadi 2001 marehemu alikuwa meneja wa shamba la Kampuni ya SAS rasmi
likijulikana kama SAS Company Ltd lililokuwa mkoani Morogoro.
KUJIUNGA NA SIASA NA KUWA MBUNGE.
• Marehemu alijiunga na The Civic
United Front - CUF Chama Cha Wananchi kama mwanachama hai mwaka 1997 na
alikitumikia chama kwa uaminifu na jitihada kubwa.
• Mwaka 2005
marehemu Salim Hemed Khamis alipitishwa na Chama Cha Wananchi CUF kuwa
mgombea ubunge katika jimbo la Chambani na alishinda uchaguzi wa Oktoba
2005 na kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.
• Mwaka 2010 alipitishwa
tena chama ili akiwakilishe katika kinyang’anyiro cha ubunge katika
jimbo hilohilo na alishinda tena na kuongoza kipindi cha pili hadi
umauti ulipomkuta.
• Alikuwa Waziri Kivuli wa Wizara ya
Kilimo,Chakula na Ushirika tangu Mwaka 2005 hadi 2010 Bunge la Tisa
lilipo maliza muda wake
NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA;
Kutokana na uwezo wake mkubwa katika masuala ya uongozi, chama
kilimpatia marehemu Salim Hemed Khamis dhamana kubwa za uongozi;
•
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa tawi la
Kimbuni tangu mwaka 1997 hadi anafariki.
• Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji jimbo la chambani na Mjumbe Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya
mkoani Pemba tangu mwaka 2005 hadi anafariki.
• Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya CUF taifa mwaka 2011 – 2012.
• Marehemu alikuwa mjumbe
wa mkutano mkuu wa Taifa 2005 hadi anafariki na mjumbe wa Baraza Kuu la
Uongozi la Taifa - CUF tangu mwaka 2011 hadi 2012.
• Marehemu
alikuwa Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi kwa ngazi ya taifa mwaka 2011
na kwa namna ambavyo alithamini masuala ya uongozi, ilipofika mwaka 2012
aliomba kupumzika wadhifa wa Ukurugenzi wa kitaifa ili aelekeza nguvu
zaidi jimboni jambo ambalo liliridhiwa na chama.
Hadi anafariki
marehemu ameacha vizuka wawili na watoto wanane.
"CHAMA CHA
WANANCHI CUF KIMEPOTEZA NGUZO MUHIMU, TUNAWASHUKURU WATANZANIA WOTE
WANAONDELEA KUTUMA SALAMU ZA POLE KWA VIONGOZI WA CHAMA NA WAFIWA".
SOURCE: Julius S. Mtatiro
0 comments:
Post a Comment