Rais na Amiri Jeshi
Mkuu, Jakaya Mrisho Kikwete amefunga rasmi mafunzo ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) ya muda mfupi kwa viongozi. Mafunzo hayo yalidumu kwa muda
wa majuma matatu na kufungwa rasmi jana, Machi 25, 2013.
Zifuatazo
ni baadhi ya picha kutoka kambi mbalimbali.
Wakiwa shambani pamoja ni
Wabunge Zitto Kabwe, Iddi Azzan, Abdallah Haji, Raya Ibrahim na Antony
Mbassa kwenye kambi ya Mgambo 835KJ.
Zitto Kabwe akijiandaa
kwenda katika gwaride la mwisho
Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzan,
wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT
Kikosi cha 835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani
Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi
Azzan pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu
mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi
Azzan, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya
Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa
Tanga.
Wabunge Halima Mdee na
Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya
muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu
JKT huko Kibaha Mkoani Pwani.
Wakiapa mbele ya kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya
JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni, Mkoa wa
Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya
Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya
Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
Mbunge wa Kiwani Pemba,
Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika
Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani
Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa
viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu
wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835
wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk
Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya
835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni
Mkoa wa Tanga. picha na Hussein Semdoe.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu,
Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda
mfupi kwa viongozi, mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi
ya Ruvu JKT.
Baadhi ya waliokuwa katika
Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
0 comments:
Post a Comment