Friday, March 29, 2013

MNAMO TAREHE 27.03.2013 MAJIRA YA SAA 13:40HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA IPONJOLA KIJIJI CHA ISANGE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. MTOTO DEBORA D/O RIZIKI, MIAKA 3, KYUSA, MKAZI WA IPONJOLA, ALIGUNDULIKA AKIWA AMEFARIKI BAADA YA KUFUKIWA KWENYE SHIMO NDANI YA NYUMBA YA BABA YAKE MZAZI ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA RIZIKI S/O SAIDI MWANGOKA, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA IPONJOLA.

TUKIO HILO LIMEFANYWA NA MZAZI HUYO TAREHE 29.11.2012. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA KINDOA KATI YA MTUHUMIWA NA ALIYEKUWA MKE WAKE ESTHER D/O MSAFIRI MWAMBENJA, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIBUMBWE-KIWIRA.

MGOGORO WAO ULIPELEKEA WAGOMBEE NANI AISHI NA MTOTO HUYO BAADA YA WANANDOA HAO KUTENGANA HIVYO TAREHE 28.11.2012 MAJIRA YA SAA 17:00HRS MTUHUMWA ALIMCHUKUA KWA NGUVU MAREHEMU KUTOKA KWA MAMA YAKE NA KWENDA NAE KWAKE KISHA KUMUUA NA KUMFUKIA SEBULENI NDANI YA  NYUMBA YAKE.

MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI KISHA KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA KUZIKWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.

TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI  WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

AIDHA ANATOA RAI KWA WANANDOA KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUTANGULIZA HASIRA NA MATUMIZI YA NGUVU.

Signed By

[DIWANI ATHUMANI – ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Post a Comment