Imeandikwa na Happiness Katabazi via blog
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema kuwa Aprili 18 mwaka huu, itaoa hukumu ya kesi ya uchochezi wizi wa malighafi za Silingi milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.
Hakimu Mkazi Victoria Nongwa aliyasema hayo saa kumi alasiri muda mfupi baada ya mashahidi watano wa upande wa utetezi waliopanda wote kizimbani kutoa utetezi na hivyo kufanya upande wa utetezi weleta mashahidi 52.
Hakimu Nongwa alizitaka pande mbili katika kesi hiyo kuwasilisha kwa maandishi majumuisho ya mwisho ya kesi hiyo Aprili 3 mwaka huu, na kwamba kesi hiyo itatajwa Aprili 4.
Kabla ya kuyasema hayo Ponda jana alipanda kizimbani na kuanza kutoa kujitetea ambapo alidai kuwa ni kweli yeye ndiye aliyetoa maagizo kwa maimau wa misikiti wawatangazie waumini wao ili waje kwenye kiwanja cha Chang’ombe Markas kwaajili ya kuja kuongeza nguvu ya kujenga msikiti wa muda katika kiwanja hicho.
Itakumbukwa kuwa mashahidi watatu wa kesi hiyo ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Ponda na wenzake 49 jumla ya mashahidi wa tatu ambao ni viongozi wa Bakwata na mkurugenzi wa kampuni ya Agritanza, walitoa ushahidi wao na kusema kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa na Bakwata ambayo ndiyo yenye dhamana ya kumiliki mali zote za waislamu lakini Bakwata ikaamua kuipatia kiwanja hicho Agritanza na Agritanza ikaipatia Bakwata kiwanja kikubwa kilichopo Kisarawe kwahiyona kusema kuwa kiwanja cha Markas siyo mali ya waislamu wala Bakwata lakini washitakiwa katika utetezi wao wanadai kiwanja hicho ni mali ya waislamu.
Sheikh Ponda aliyekuwa akiongozwa kutoa utetezi wake na wakili wake Juma Nassor na Njama mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa alieleza ni yeye ndiye aliyetoa maelekezo hayo ya kuwataka waislamu wote wafike katika eneo hilo ili wajenge msikiti wa muda na kwamba waislamu hao waliitikia wito na kwamba kuanzia asubuhi ya saa moja hadi saa 12 jioni ya Oktoba 12-14 yeye na waislamu hao walikuwa wakijenga msikiti huo ndani ya kiwanja hicho ambacho ni mali ya waislamu.
“Kiwanja hicho ni mali ya waislamu na kiwanja hicho tulipewa sisi waislamu na serikali ya Misri tena wakati huo waislamu wote tulikuwa chini ya East Africa Muslim Welfare,lakini baadae taasisi hiyo ilifutwa na serikali ndiyo ikaanzishwa Bakwata…kwahiyo kufutwa kwa taasisi ile hakumaanishi mali zilizokuwa chini ya taasisi zake nazo zimefutwa,kinachofanyika pale ni majukumu ya taasisi yale yanakuwa yamesimama na mali zake zinabaki kuwa ni za wanachama wake wa taasisi hiyo iliyofutwa ”alidai Sheikh Ponda
Hata hivyo alikanusha mashitaka yote yanayomkabili na kusema hafahamu ni kwanini upande wa Jamhuri umemfungulia mashitaka hayo kwa sababu hata hilo kosa la wizi wa malighafi, mahakama ilipaswa ihamie kwenye eneo la tukio iende ikashuhudie kama wale Waislam niliokuwa nao walichukua malighafi za kampuni ya Agritanza ili kujengea msikiti wa muda.
Akielezea jinsi alivyokamatwa na askari, Ponda alidai Oktoba 16 mwaka jana, saa nne kasoro wakati akiingia ndani ya msikiti wa Tungi uliopo Temeke , kabla ya kuingia ndani alisikia sauti ya mtu ikimuita na mtu huyo alikuwa ndani ya gari, akawataka watu hao wamfuate nyuma.
“Nilipoingia msikitini nikasikia sauti ya magari nikatazama nikaona magari matatu aina ya Land Cruiser yana askari wa kikosi cha FFU wakiwa na silaha na mabomu na wale askari walingia ndani ya msikiti wakiwa wamevaa viatu wakanivamia na kuniangusha chini, wakanitoa ndani ya msikiti kwa mtindo wa kuniteka nyara na kunikimbiza kwenye gari lao kwa kasi,”alidai Sheikh Ponda.
Aliendelea kudai kuwa walimepeleka katika kituo cha polisi Chang’ombe na, “wakanieleza kosa langu na wakaniambia mimi siyo raia wa Tanzania, ni kwa nini nisiende kufanya vurugu Burundi? Mi nikawaambia ni raia wa Tanzania,” alidai Ponda.
Akijibu maswali ya wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka kuwa hakuona ni kosa kwa yeye kuita Waislam waende kujenga msikiti wa muda katika eneo lile ambalo si mali ya Waislam, Ponda alijibu kuwa, ‘Sikiliza Kweka, mimi nimeanza mijadala tangu enzi Serikali ya rais Julius Nyerere, kwa hiyo nina uzoefu na huo siyo uchochezi,” alidai Ponda.
Kwa upande wake mshitakiwa wa tano, Mkadamu Abdallah akijitetea yeye alidai kuwa hafahamu hicho kiwanja kiliuzwa kwa nani, na wala hajawai kutoa maelezo polisi na hafahamu kama Ponda alienda kwa Mufti wa Tanzania, Sheikh Simba kumuuliza ikiwa kiwanja hicho kimeuzwa.
Hata hivyo, wakili Kweka alipomtaka Mkadamu arejee maelezo yake aliyoyatoa polisi ambayo yamepokelewa mahakamani kama kielelezo.
Ndani ya maelezo hayo, Mkadamu alikiri kufahamu kuwa kiwanja kile kimeuzwa kwa Agritanza na BAKWATA na kwamba yeye na Waislam wenzake walienda katika kiwanja hicho na kuanza kujenga msikiti wa muda.
Mkadamu aliishia kudai kuwa maelezo hayo si yake.
Oktoba 18 mwaka jana, kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapa kwa mara ya kwanza ambapo washitakiwa wanakabiliwa na jumla ya makosa matano ambayo ni kula njama kutenda kosa, kuingia kwa jinai, kujimilikisha kwa nguvu kiwanja hicho na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. milioni 59 na uchochezi.

0 comments:
Post a Comment