Sunday, February 3, 2013

WAELEWE MATAPELI WALIOKUBUHU HAPA DAR ES SALAAM.
IMENITOKEA MM LEO 02/02/2013 KWA MARA YA PILI

Kuna utapeli fulani unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa sana na wanaendelea kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa.

Nadhani matapeli hawa wanatumia ujinga wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo kabla ya kusema au kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa haraka kwa njia yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili.

Utapeli huu sio mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu na meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/munayefahamiana na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia.

Baada ya hapo wanaanza kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka kwa madai kuwa mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza kuleta uswahili hivyo kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona ni vema akutumie wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission kubwa ambayo huwapa ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema wanafanya kazi na shirika la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani (UNHCR) na wako Kigoma.

Zaidi ya mwaka mmoja sasa nikiwa ofisini walinipigia na aliyekua anaongea name alianza kwa kujitambulisha kama graduate wa kitivo cha uhandishi cha chuo Kikuu Mlimani na kwamba tulisoma wote mwaka mmoja wakati nikisoma degree ya kwanza lakini huenda simkumbuki kwa sababu nilikua kiongozi wa fellowship na siwezi kuwa nakumbuka wote niliokua nawaongoza. Yeye alikuWa fellowship.  Alikua akiongea kwa kicheko na “bwana yesu” asifiwe nyingi ili
kunionesha ni kwa kiasi gani namfahamu na tunafahamiana. Kwa bahati mbaya wakati ananipigia nilishasikia kwa umbali juu ya utapeli huo ambao kwa kipindi hicho ndio ulikua umeanza tu na kushika kasi huku watu wengi wakiwa wamepoteza mamilioni. Hivyo alipoanza kuongea ujinga wake wa kunipa commission and all that, nilimwambia tu kuwa sina muda wa kujihusisha na biashara aliyokua “anataka kunisaidia ili nipate pesa za bure”, kwa haraka na bila jasho. Alikua disappointed sana kwa jibu langu hasa kutokana na muda mrefu alioutumia kunishawishi nikubali “msaada aliokua ananipa kama mpendwa mwenzake”.




Leo asubuhi majira ya saa nne nilipokea simu kwenye line yangu ya tigo na number iliyonigia ni 0717-093260. Mtu aliyenipigia alikua anaongea kwa uchangamfu mkubwa na kwa furaha huku akitaja majina yangu yote na kuniuliza iwapo kwa sasa niko DSM au nimesafiri. Aliniambia kuwa kafurahi kusikia kuwa niko DSM kwani ndipo zilipo ofisi zao na kwamba alitaka kuniunganisha zao ili nikachukue mzigo ambao utakua na cha juu kizuri sana. Nilipoona anaendelea nilimuomba ajitambulishe.... akaniambia anaitwa Lameck na kuwa alishafanya kazi Planet International hapa chuo kikuu. Alipotamka hivyo nikaanza kupata ukakasi kwani hapajawahi kuwa ofisi ya kampuni hiyo hapa Mlimani. Nikamuuliza yuko wapi kwa sasa na kwa msisitizo akanijibu kuwa kwa sasa yuko Serengeti National Park.

Nikamuuliza iwapo anafanya kazi na TANAPA... akasema hapana bali yuko na shirika moja la Kijerumani  linalojishughulisha na wanyamapori... na akijua kuwa niko Chuo Kikuu alitafuta style nzuri ya “kuniingiza alipokusudia” ...maana alianza kunieleza kuwa shirika lao linafanya “tafiti za wanyama pori katika mbuga yetu ya Taifa kubwa sana”. Bado nikiwa najaribu kuunganisha “idadi ya nukta kadhaa” akaniona mjinga sana na kuanza kunielezea jinsi wanyawa walioko Serengeti wanavyo migrate kila mwaka kwenda Kenya... na kuwa wanahama wengi kama elfu mbili hivi... (nikapata nukta nyingine)... then nikaingilia na kumsaidia kuwa hawavuki kwa maelefu bali ni zaidi ya milioni moja wanahama na kurudi kila mwaka. Pomaja na utafiti kazi nyingine wanayofanya ni pamoja na kutoa chanjo kwa wanyama hawa maana wanaporudi wanakua wamerudi na magonjwa toka Kenya.

Hapa ndipo alipopotea njia zaidi kwani kati ya jambo ninalolijua kwa mapana kidogo ni hii movement ya wild beasts, zebra na wengine walioko Serengeti . Nikamuonesha kushangaa kuwa wanawezaje kuwapa chanjo  wanyama wengi namna hii (na kumuonesha najua chanjo ni nini nikajifanya mhaya kidogo na kutamka vaccination)... akaanza kujichanganya kuwa wao wana njia tatu za kutoa chanjo maana ni kweli kuwa wanyama ni wengi... kwanza wanatengeneza majosho/mabwawa/madimbwi ambayo wanaweka dawa na hiyo wale wanyama wanapokua wanarudi wanatumbukia na hivyo automatically wanakua wamepata chanjo. Hapa akachemka zaidi...nikamuuliza hivi kuogesha ng’ombe kwenye majosho ni chanjo au ni kuua kupe na viroboto? Nikamuuliza kuna chanjo inafanyika juu ya ngozi?... alipoona hana majibu akauma maneno mawili-matatu halafu akasema njia ya pili wanayotumia ni kuwakamata wale wakubwa kama tembo na wengine na kuwapiga sindano za chanjo.... nikajizuia kucheka. Alipoona swali lingine linafuata kabla hajaanza kuningiza kwenye “undani/details za deal” lenye commission ...akaomba udhuru kidogo kuwa bosi wao kaingia ofisini mara moja na hivyo atanipigia baadaye kidogo...akakata simu na ukawa ndio mwisho wa mawasiliano

Alipokata simu tu nikam-text kuwa angeendelea tu na ujinga wake maana nawafahamu vema na wanachokifanya... na huo ukawa ndio mwisho wa ile namba kupatikana hewani baada tu ya ujumbe wangu kuwa delivered.

Ushauri Kidogo:

  • Unapojikuta kwenye mazingira ya mtu kujitambulisha kwako kwa nguvu kubwa huku ukiwa humfahamu, mpe nafasi ya kuongea
  • Unapojikuta kwenye mazingira ya kudanganyika kuwa unaweza kunufaika na kupa utajiri kirahisi kwa mtindo wa ki_DECI_DECI au kimuujizaujiza, usichanganyikiwe na kuanza kuutazama huo muujiza kama ndio umeshakufikia. Utafanya la muhimu sana iwapo utaruhusu akili yako kufanya kazi na kutafakari vema kila unachokiona au kukisikia
  • Kama unaweza, ni vema kurecord mazungumzo ambayo una wasiwasi nayo
  • Kama unaweza, una nafasi, na una matumaini kuwa polisi wanaweza kuwa na msaada kwenye hili, basi wasikilize watu hawa na kutafuta msaada wa polisi kwani utaokoa na wengine wasidanganyike
  • Tambua tu kuwa watu hawa wana mtandao mkubwa sana na mara nyingi wanafanya mambo yao wakiwa na taarifa za kuwatosha na wamejipanga. Unaweza ukawa kwenye mstari mwembamba sana unaotofautisha ukweli na uongo
  • Kwa nini bado makampuni ya simu yanaruhusu simu kutumika ikiwa haijasajiliwa? Na kama imesajiliwa, je wale wanaoandikisha hizi simu, wana ujuzi wowote wa kugundua kitambulisho halali na ambacho ni fake watu wanavyovitumia kusajilia simu zao?

Ufahamu na Akili tuliyonayo ukitumika vema bil haraka ya mafanikio tunaweza kukabiliana na changamoto nyingi za kitapeli tunazokumbana nazo!

0 comments:

Post a Comment