SPIKA wa Bunge, Anne Makinda
• Mangula atoboa siri ya uteuzi wake
na Mwandishi wetu
|
|
|
SPIKA
wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaweza
kujiondoa chenyewe madarakani kutokana na tabia ya baadhi ya viongozi
kutanguliza maslahi binafsi badala ya chama na wananchi kwanza.
Makinda alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwasalimu wajumbe wa mkutano wa
Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Njombe, waliokutana mjini hapa.
Alisema utapeli ndani ya CCM unatisha na watu hawataki kujenga utamaduni
wa ujamaa na kujitegemea na kusisitiza iwapo wanachama watashindwa
kujitegemea, chama kitakufa.
Alisema hata rushwa kwenye uchaguzi wa CCM inachangiwa na baadhi ya
viongozi wasiopenda kufanya kazi na kutegemea kuchuma pesa za rushwa
kutoka kwa wagombea.
“Rushwa ndani ya chama inatokana na tabia hii ya watu kushindwa kufanya
kazi halali za kujitafutia kipato na kuishia kuwarubuni wagombea na
kuwaomba fedha kwa ahadi ya kuchaguliwa. Iwapo wana CCM wataendelea
kuomba fedha katika uchaguzi ni mwanzo wa kuua chama na hata vyama vya
upinzani haviwezi kuiua CCM ila CCM itajimaliza yenyewe kwa tabia yake,”
alisema.
Alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya wapiga kura wa jimbo
lake ambao wamekuwa wakimchangamkia na kumsalimia na mwisho wa salamu,
huishia kuomba pesa.
Makinda amewataka viongozi wa CCM kurejea misingi ya kiapo cha mwachama
na kukifanyia kazi kiapo hicho ambacho kinatamka wazi kuwa sitatumia
cheo changu kwa maslahi yangu na iwapo kiapo hicho kitaendelea kukiukwa
kwa baadhi ya viongozi wanaochaguliwa kugeuza nafasi zao ni mitaji ya
kuombaomba fedha kwa wabunge, chama hicho hakitadumu.
“Mimi mwenzenu jana baada ya kumaliza mkutano wa mapokezi ya Mangula
nilianza kucheza ngoma na muziki na wananchi waliofika katika mapokezi
hayo, cha ajabu wengine walikuwa kukisalimia na kuniomba pesa ....sasa
hii ni hatari sana kama watu wamekuja wenyewe katika mapokezi baada ya
kumaliza mkutano, wanamvamia mbunge na kumwomba pesa,” alisema Makinda.
Kutokana na hali hiyo, Spika Makinda aliwataka wanachama wa CCM kufanya
kazi na kuwa na shughuli nyingine za kuwaingizia kipato badala ya
kuendelea kuwavizia wabunge na kuwaomba pesa na wasipopewa wamekuwa
wakiwachukia na kukichukia chama.
Makinda aliwataka pia wajumbe wa mkutano huo kuwa na miradi ya kiuchumi
au kujiunga katika kilimo badala ya kuendelea kuomba fedha kwa wabunge.
Alisema hivi sasa watu wamechoka kuombwa fedha na hata waliokuwa
wakikisaidia chama, pia wamechoka hivyo lazima CCM ijitegemee kwa kuwa
na miradi ya kiuchumi.
Wakati huohuo wajumbe wa mkutano huo wamemchagua kwa kura za kishindo
mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, kuwa mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa toka wilaya ya Njombe baada ya kupata kura 37 kati ya kura
45 zilizopigwa kati ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe.
Akitangaza matokeo hayo katibu wa CCM mkoa wa Njombe, Hosea Mpagike,
alisema katika wilaya ya Ludewa kulikuwa na wagombea watatu katika
nafasi hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa, Matei Kongo,
aliyepata kura 25 na Damiani Mwapinga aliyepata kura 24 na washindi ni
wajumbe Filikunjombe na Kongo.
Walioshinda katika ya wilaya ya Wanging’ombe na kura zao kwenye mabano ni Anaupendo Gombela (36) na Happiness Bomba (31).
Washindi kutoka wilaya ya Makete ni Elizabeth Haule (28) na Francis Chaula aliyepata kura 23.
Wakati huohuo, mbunge wa Ludewa, Filikunjombe, amewalipua watendaji
wabovu serikalini, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, bara, Philip
Mangula.
Filikunjombe ambaye alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano wa
mapokezi ya Mangula mkoani Njombe, alisema kuwa masikitiko ya wananchi
juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya
chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na
kusababisha wananchi kukichafua na kukichoka chama tawala.
Hivyo alisema kuwa imani ya wana CCM kwa safu mpya ya uongozi chini ya
Katibu Mkuu Abdalaman Kinana na Makamu Mwenyekiti Mangula na Makamu wake
Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein, na viongozi wengine ndani ya CCM ni
matumaini mapya kwa wana CCM na tishio kwa vyama vya upinzani.
“Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe, chama chetu CCM ni
chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete, Mangula na
Kinana ni safu ya uhakika na itakiwezesha kuendelea kuaminiwa zaidi na
Watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika
katika nafasi zao,” alisema.
Kwa upande wake Mangula mbali ya kusifu mapokezi aliyopata, alitoboa
siri ya uteuzi wake kwamba alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi huo na
kwamba alishangaa sana kupokea simu ya Rais Kikwete na kumueleza kuhusu
kusudio la uteuzi huo.
“Kweli mimi nilikwenda Dodoma katika Mkutano Mkuu wa CCM kama mualikwa
ila nikiwa hotelini nilipokea simu ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais
Kikwete, akiomba kuniteua kuwa Makamu Mwenyekiti na baada ya kwenda
ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana
Mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na
sitawaangusha,” alisema Mangula.
Alisema hatafanyakazi kwa kulipa kisasi kwa wana CCM waliokuwa hawaelewani naye. | | |
|
0 comments:
Post a Comment