Questions
|
||||||
Session No | Question No | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
---|---|---|---|---|---|---|
7 | 99 | PRESIDENT'S OFFICE (PUBLIC SERVICE MANAGEMENT) | Employment | 19 April 2012 | ||
Principal Question No | ||||||
Serikali imeazimia kujenga Vituo vya Afya kwa kila kijiji na shule za
sekondari kwa kila Kata, hata hivyo shule za Kata hazina walimu wala vifaa vya kufundishia na pia zahanati zetu hazina watumishi wa kutosha na kwamba miaka ya nyuma Serikali iliazimia kuwaajiri kwa mkataba maalum watumishi wa Elimu na Afya waliostaafu lakini zoezi hilo likasitishwa. Je, Serikali itarudisha lini ajira hizo za mkataba kwa kada hizo zenye upungufu mkubwa wa watumishi? |
||||||
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #99 SESSION # 7 | ||||||
|
||||||
WAZIRI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salome Daudi Mwambu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuwaajiri watumishi kwa mikataba umeanisha katika Kanuni D. 28 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo la 2009 na waraka wa Rais, Na. 1 wa mwaka 1998. Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo haya ajira za mikataba hasa katika maeneo yenye mahitaji makubwa kama vile Afya na Elimu zitaendelea kutolewa kwa mujibu wa Kanuni nilizozitaja. |
0 comments:
Post a Comment