Meneja Mkuu wa Multichoice
Tanzania Bw. Peter Fauel, akitangaza Punguzo la Asilimia Kumi ya Malipo
ya mwezi kwa wateja wa Televisheni kwa Vipindi vya DStv likaloanza hapo
kesho, ambapo amesema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia
huduma za Matangazo ya Televisheni ya kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia
amesema Offer hiyo ya Punguzo la bei ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha
fadhila kwa wateja wake kuelekea katika kipindi cha maadhimisho ya
sikukuu za mwisho wa mwaka. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Multichoice Barbara Kambogi na Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo
Bi. Furaha Samalu.
Meneja Masoko wa Multichoice
wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu akitoa ufafanuzi kuwa katika kipindi
hiki cha kuelekea matumizi ya mfumo wa Digitali DStv kwa kuwajali wateja
wake imepunguza gharama za kuunganishwa ambapo sasa ni kwa shilingi za
Kitanzania 169,000 unaweza kusheherekea msimu wa sikukuu na DStv.
Kampuni ya MultiChoice imetangaza
punguzo la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa wateja wa televisheni kwa
vipindi vya DStv litakaloanza kesho Novemba 15, 2012.
Meneja Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Peter Fauel alisema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma za matangazo ya televisheni ya kituo hicho kwa gaharama nafuu.
Fauel alisema kwa wateja watakaokuwa wamelipia tayari huduma hiyo ndani ya mwezi huu, wataendelea kutumia hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha, kisha wataanza na bei mpya ya punguzo kuanzia mwezi unaofuata ila wahakikishe huduma yao kutokatika.
"Tumedhamiria kuwapunguzia wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida," alisema Fauel.
Meneja mkuu huyo alisema, kuwa kama kawaida yao huwapa wateja wao unafuu wa bei kulingana na kipato chao, hivyo punguzo hilo litawanufaisha kwa kiwango kikubwa ili kila mmoja afaidi burudani.
Alisisitiza kuwa DStv itaendelea kuwapatia Watanzania na Waafrika kwa ujumla vipindi vyenye ubora kwa vile wamewekeza katika vipindi vipya.
Kwa wateja watakaonufaika na ofa hii, wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa 150,000 kwa mwaka!
Fauel akaongeza kwamba “Tunawaahidi wateja wetu huduma bora na kwamba kwetu mteja ni mfalme. Mtandao wetu wa usambazaji unazidi kupanuka na sasa tupo kila mkoa wa nchi. Pia tunafurahi kwamba sasa tuna ofisi zetu Kariakoo na supermarket ya Uchumi iliyopo barabara ya Pugu. Hii itawarahisishia wateja wetu kupata bidhaa na huduma zetu kwa haraka zaidi.
---
via Zainul Mzige, mohammeddewji.com/blog

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Multchoice Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akiwahakikishia wateja wa
DStv kuwa sasa kampuni hiyo imezidi kuboresha huduma zenye viwango vya
hali ya juu na kuwataka wazazi kutumia fursa hii ya punguzo la bei ya
kuunganishwa ili watoto wao waweze kushuhudia vipindi mbali mbali vya
kuelimisha na kuburudisha ikiwemo filamu kali, katuni maridadi, michezo
mbalimbali katika kipindi hiki cha likizo kwa watoto wao na kuwa huu
ndio sasa muda muafaka kwa kujipatia DStv.
Meneja Mauzo wa DStv Tanzania
Bw. Salum Salum akifafanua kuwa Multichoice imepanua wigo wa kutoa
huduma kwa wateja ambapo sasa wanamawakala 200 nchini na kuwataka
wanapokwenda kulipia Ving'amuzi vyao ni lazima wahakikishe vimewashwa
ili kurahisisha kufanyika kwa huduma hiyo pia amesema wateja wa DStv
wanaweza kufanya malipo ya huduma hiyo kupitia simu za mkononi na
ukizingatia kampuni hiyo imeongeza maeneo ya kutoa huduma ikiwemo Uchumi
Super Market, Kariakoo na Mlimani City kwa wakazi wa Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment