Mmoja wa Maofisa wa Polisi akielekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha
Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga (tatu shoto), ACP Kilonzo kutoka
makao makuu ya jeshi la Polisi (mwenye miwani) pamoja na ASP Msuyale (
wa tatu mstari wa nyuma) wote kutoka nchini Tanzania, kuhusiana na mambo
ya usalama barabarani.
Maofisa hao wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka nchini Tanzania
walikuwa nchini Ujerumani kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja (21/10 -
27/10/20120), katika jimbo la Lower Saxon, ambapo pia walitembelea Mji
mkuu wa jimbo hilo Hannover, Neunberg, na Gottingen.
Aidha ziara hiyo ilihusisha mambo mbalimbali ya usalama barabarani
ikiwemo kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga
picha, na rader ya kawaida, ukaguzi wa malori ya mizigo na mambo
mengine mengi..
Mmoja wa Maofisa wa Polisi (mwenyeji) akiwaelekeza jambo kwa Kamanda Wa
Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja
na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) namna ya matumizi mbalimbali
ya usalama barabarani.
Mmoja wa Maofisa wa Polisi akimuelekeza Kamanda Wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, SACP Mohamed Mpinga namna ya kuangalia upimaji mwendo kasi
kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha kuhusiana na uendeshaji magari
barabarani.
Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga,ACP
Kilonzo pamoja na ASP Msuyale wakielekezwa namna ya leseni za madereva
zinavyokuwa.
Maofisa wa juu wa kutoka jeshi la polisi nchini Tanzania, Kamanda Wa
Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na
ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) wakiwa katika picha ya pamoja na
wenyeji wao.Picha zote kwa hisani ya SACP Mohammed Mpinga - CO Traffic.
picha zimeshirikishwa na Ahmad Issa Michuzi, michuzijr.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment