Na Ben Komba-Pwani
Kupingana
na zoezi la sensa ni kupingana na amri halali ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kutokana na mamlaka aliyopewa,
kabla ya kuanza zoezi hilo anatakiwa kutoa Amri kama Rais ya kutangaza
kufanyika kwake, muda, mahali na wahusika katika sensa.
Hayo
yamesemekana katika kikao kati ya madiwani na kamati ya uratibu wa
sensa Wilayani Kibaha, ambapo Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya
Kibaha, Bi. Salama Mangara amewaambia madiwani kuwa sheria hii inatamka
kufuatana na sheria Namba 1 ya Mwaka 2002 kwa ajili ya zoezi la sensa ya
watu na makazi kifungu cha 14.
Bi.
Mangara ameongeza kuwa makosa ambayo mtu anaweza kujikuta yupo hatiani
iwao atakayoyafanya ni pamoja na kumzuia Msimamizi, Mdadisi, Karani wa
sensa kutekeleza majukumu yake, kukataa au kuacha kwa makusudi kujaza
fomu au nyaraka yoyote iliyokabidhiwa kwake kwa lengo maalum, kukataa
kujibu maswali aliyoulizwa, kutoa taarifa za uongo au kukiuka kifungu
chochote cha sheria atapata adhabu ya kifungo miezi sita na faini
shilingi laki 6 za kitanzania.
Bibi
. Mangara amesisitiza kwa mantiki hiyo, ni jukumu la kila mmoja
kutimiza wajibu wake na kutoa ushirikiano unaostahili katika zoezi la
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Mratibu
wa sensa ya watu na makazi wilayani Kibaha, Bi. Letti Shuma akizungumza
na madiwani amewataka madiwani kwenda kutengeza mazingira kwa
kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wao wa kushiriki kwao zoezi la
sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika tarehe 25 na 26
mwezi huu na kuendelea kwa siku saba.
Bi.
Shuma amesema malipo yote kwa wahusika wa sensa zimelipwa kiakmilifu
tofauti na maeneo mengine ambayo yalikumbwa na mizozo, kilichobakia kwa
sasa ni kwa wasimamizi na makarani kulipwa fedha kabla ya kuanza
shughuli hiyo,zoezi ambalo limezorota kutokana na matatizo ya kibenki,
lakini taarifa za uhakika ambazo anazo mpaka anapoongea na wawakilishi
hao wa wananchi kua fedha hizo zimeshafika hazina tayari kwa zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment