Muda
mchache uliopita tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa
kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye klabu yake Azam jana
imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya Simba.
Katika
mazungumzo hayo Mrisho Ngassa amesema kwamba yeye binafsi hajapata
taarifa rasmi kutoka kwa klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba.
"Kiukweli hizo taarifa mie nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti
lakini muajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia
huu utaratibu sidhani kama ni sahihi, wanawezaje kuniuza timu nyingine
bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu katika hiyo timu nyingine
nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa kuamini kama Azam
watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba Ngassa
tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au
kukataa.
Ngassa
akaendelea alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa
kuna hali ya kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na
mshabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote
nilichokaa pale. Unaweza ukajiuliza kwanini mimi mpaka jana kwanini
mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi kwangu au ninakuwa na ukaribu
nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa baraka zote na klabu
yangu, yaani niliondoka vizuri. Azam walikuja wakaongea na Yanga
wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa
chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje jana wao
wameshindwa kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa
kuninunua kutoka Yanga. Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba
ingebidi na mie nipewe taarifa ili kuweza kukubaliana mahitaji yangu
binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini sivyo walivyofanya."
Alipoulizwa
kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu
hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili
kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa
mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo.
Taratibu lazima zifuatwe na kuniuza kama kiroba cha mchele, kwa hali
ilivyo mpaka sasa sitoweza kujiunga na Simba"
By Aidan Charlie
By Aidan Charlie
0 comments:
Post a Comment