Mtu mmoja anadaiwa
kufa kwa kupigwa risasi kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya
kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu
ya machozi waandamani wa CHADEMA mjini Morogoro.
Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa jana. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi. (MrokiM blog)
Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa jana. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi. (MrokiM blog)
Askari wa Kikosi cha kuzuia fujo FFU wakitoa onyo kwa waandamanaji kutawanyika (picha via Habari Mseto blog)
picha via WanaBidii google forums
picha via WanaBidii google forums
picha via WanaBidii google forums
Huyu
ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada
ya kutandikwa risasi na Polisi kuzuia maandamano ya CHADEMA (picha
Father Kidevu blog)
Huyu
ni mwananchi aliyeuawa na polisi kufuatia maandamano ya amani ya
CHADEMA leo asubuhi... Alikuwa ni muuza magazeti ambaye hakujihusisha
hata na maandamano. Wengine watatu wamejeruhiwa kwa risasi. (picha:
CHADEMA Blog)
Msimamo wa JOHN MNYIKA kuhusu vurugu, risasi, kujeruhi na “kuua” Morogoro!
Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.
Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa.
States captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot. Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.
John John MNYIKA,
27 Agosti, 2012
0 comments:
Post a Comment