Mheshimiwa
Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa akitoa mchango wake kuchangia ujenzi
wa hosteli za wanafunzi wa kike kupitia kampeni ya Elimu yao Wajibu
wetu, kampeni inayoendeshwa na mabalozi wa Mamlaka ya Elimu (TEA).
**********
Kikundi
cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana
kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania
billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia
wasichana wa shule za sekondari 1,504.
Kikundi
hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji
wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari
(Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006)
na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya
kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na
TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.
Mabalozi
hao wamefika bungeni na baada ya kutambulishwa wameendelea na zoezi la
kuchangisha fedha kutoka kwawabunge wa bunge hilo.
Mratibu wa kampeni ya Elimu yao Jukumu letu Rebeca Gyumi akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda jinsi
harambee ya uchangiaji mabweni inavyoendeshwa na makusudio ya harambee
hii. TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi za kitanzania bilioni
2.3 zitakazotumika kujengea hosteli 30 katika mikoa minane nchini.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mh.
Margreth Sitta akitoa mchango wake kwa TEA katika kuchangia harakati za
Mamlaka ya Elimu Tanzania kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakuwa na
makazi salama.
Mheshimiwa Vicky Kamata (MB)(Katikati) akijaribu moja ya huduma ya kuchangia kampeni hii ya ujenzi wa mabweni kulia
kwake ni Nancy Sumari Miss Tanzania 2005 na kulia kwake ni Faraja
Nyalandu Miss Tanzania 2006 ambao ni mabalozi wa kampeni hii.
Mh.
Sophia Simba Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na Watoto akitoa
mchango wake kuchangia kampeni hii bungeni. Ili kuchangia pia unaweza
kutuma neno CHANGIA TOFALI kwenda namba 15564 ambapo utakatwa shilingi
250 tu za kitanzania.
Mbunge
wa Kilosa Mh. Mustapha Mkulo (MB) akitoa mchango wake kuchangia kampeni
hii. Mabalozi wa harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa
hosteli za watoto wa kike waliamua kwenda bungeni kuwaomba wabunge wachangie kampeni hiyo.
0 comments:
Post a Comment