Waziri
Mkuu Mizengo Pinda hii leo amewaongoza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mara
katika Mazishi ya Mwalimu James irenge aliyemfundisha Baba Wa Taifa
Hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1935 katika Shule ya Msingi Mwisenge
iliyoko katika Manispaa ya Musoma. Marehemu Mwalimu Irenge amezikwa leo
katika kijiji alichozaliwa cha Busegwe Nyanza, Wilayani Butiama kwa
heshima zote za Kiserikali.
Marehemu alizaliwa mwaka 1892 katika kijiji cha Busegwe, mwaka 1924-1925 alisoma Standard two Busegwe, Mwaka 1927 alisoma darasa la pili, Mwisenge middle school, Mwaka 1932 alijiunga na Chuo cha Ualimu Mpwapwa, 1934 alifundisha Chuo cha Ualimu Mpwapwa, 1935 alihamia Shule ya Msingi Mwisenge ambapo alikutana na Hayati Baba wa Taifa na kumfundisha darasa la tatu na la nne akiwa anaishi naye Mtaa wa Mkinyerero, Mwisenge. Marehemu alistaafu mwaka 1970 akiwa mkaguzi wa Shule za Msingi katika Wilaya za Geita na Biharamuro.
Baada ya kustaafu Hayati Baba wa Taifa alimshauri aanzishe Kijiji cha Ujamaa ambacho kiliitwa Ihayabuyaga huko Geita, Mwanza. Mwaka 1980 alirejea nyumbani kwake Mwisenge. Marehemu ameacha Mjane, watoto kumi na wajukuu 35, vitukuu 4 na vilembwe wawili.
Paschal Michael, Musoma.
www.wotepamoja.com

0 comments:
Post a Comment