Baadhi ya wananchi wakipita kutambua miili ya marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitalini ya Geita. (Picha na Victor Eliudi). |
****************************
Na Mwandishi Wetu, Geita
WATU 11 wamekufa papo hapo na wengine 12 wamejeruhiwa vibaya katika
ajali iliyotokea mkoani hapa, ikihusisha magari mawili ya abiria aina ya
Corolla, maarufu kama “Michomoko” yenye namba za usajili T 813 AZE na
T344 BPL yaliyogongana uso kwa uso.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 6:30 mchana eneo la Chibingo nje kidogo ya
mji wa Geita wakati gari lenye namba T344 BPE, lililokuwa likitokea
Geita kwenda na Katoro lilipojaribu kuipita gari yenye namba T421 BHS na
ndipo lilipogongana ana kwa ana jingine lenye namba T 813 AZE
lililokuwa kwenye mwendo kasi likitokea Katoro kwenda Geita.
Mashuhuda wa ajari hiyo ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini,
walidai kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi wa madereva wa magari
hayo.
Akithibitisha kuwepo kwa ajali hiyo, Mkuu wa Polisi Kitengo cha Usalama
Barabarani Mkoa wa Geita, John Mfinanga, alidai kuwa waliokufa kwenye
eneo la tukio ni tisa na wengine wawili walifia hospitali ya Wilaya ya
Geita wakati wakipatiwa matibabu.
Alisema kati ya waliokufa wanaume ni watano, wanawake watatu na watoto watatu akiwemo dereva wa moja ya magari hayo.
Aidha baadhi ya marehemu wa ajali hiyo ni watoto: Amin Aliud, Emison Eliud, Sala Eliud pamoja na baba yao Eliud Ngovongo.
Wengine ni Ummy Charles, Masasila Benjamin na dereva wa moja ya magari hayo aliyetambulika kwa jina moja la James.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Omari Manzie,
alifika katika chumba cha kuhifadhia maiti ilipo miili hiyo na kuahidi
kuwashughulikia madereva wote watakaobainika kuvunja sheria za usalama
barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
0 comments:
Post a Comment