Na Gideon Mwakanosya, Songea.
MWALIMU mmoja wa jinsia ya kike
aliyefahamika kwa jina moja la Kahimba wa shule ya msingi ya
Kambarage iliyopo Kata ya Msamala katika Halmashauri ya Manispaa ya
Songea Mkoani Ruvuma amajeruhiwa vibaya kwa kupigwa sehemu
mbalimbali za mwili na kundi linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa
shule hiyo ambao wanadaiwa kuwa na hasira baada ya walimu wengi wa
shule hiyo kutoonekana eneo la shule kufuatia mgomo wa chama
cha Walimu (CWT).
Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambarage Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa ni udhalilishaji mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.
Ndunguru alisema kuwa yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma kutokana na Serikali kushindwa kutimiza ahadi yao wanayodai.
Alifafanunua kuwa inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu mbalimbali za mwili na baadaye alifanikiwa kukimbia.
Kwa upande wa baadhi ya walimu wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.
Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.
Shule zilizotembelewa na waandishi wa habari ambazo hazikuwa na walimu kabisa ni Shule za Msingi za Matarawe, Mwembechai, Sabasaba, Mkombozi, Kawawa, Mfaranyaki, Majengo, Songea, Kambarage, Msamala na Majimaji na shule za sekondari za matarawe, Mfaranyaki, Shule ya wavulana Songea na Shule ya wasichana songea.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Majimaji Tamimu Ajali anayesoma darasa la tano ameiomba Serikali kuharakisha kutekeleza madai ya walimu wanayodai kwani bila kufanya hivyo kunauwezekano mkubwa wa kushuka kwa kiwango cha Elimu hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wapo kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.
Tamimu alisema kuwa ni vyema serikali ikatambua umuhimu wa mwalimu kwa kumuuongezea mshahara sawa na taaluma zingine muhimu kwa mfano. Wanajeshi, Madaktari,Wauguzi na wahudumu wa afya.
Afisa Elimu wa halmashauri ya Manispaa ya Songea Fulgensi Mponji amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa walimu amabapo alisema Manispaa hiyo ina shule 72, Sekondari za Serikari 23, Shule za seskondari za binafsi 13 ambazo idadi kubwa ya walimu hawakuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.
Alisema kuwa tayari ameshawaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu Elimu kata wote kukutananao katika shule ya msingi Mfaranyaki kwa lengo kuwakutanisha walimu ili kuzungumzia namna ya kutatua tatizo hilo.
Naye Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma Luya Ng`onyani alisema kuwa mgomo huo ni halali na umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 80 (1) ambapo hatua ya kwanza CWT kwa niaba ya wanachama tayari imetekeleza kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu CMA No: 1.
habari via dj-sek.blogspot.com

Wanafunzi
wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya
msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi
jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za
Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka
serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.
Wanafunzi
wa shule za Makuburi na Mabibo, wakiwa chini ya mwembe, jana asubuhi
Jumatatu Julai 30. Walimu wengi hawakuingia madarasani kufundisha jana
wakiitikia mwitoi kutoka chama cha walkimu nchini kilichowataka
kutofanya kazi leo Jumatatu na kuendelea hadi madai yao kuhusu maslahi
yatakaposhughulikiwa na serikali.
Baadhi
ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makuburi, wakijisomea
baada ya walimu shuleni hapo kugoma kufundisha jana Julai 30, 2012.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye hata hivyo alikataa kutaja jina lake,
alisema walimu walifika lakini hawakufanya kazi wakiunga mkono agizo la
rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba, aliyewataka walimu wote
kushiriki mgomo usio na kikomo kuanzai leo Jumatatu.
Afisa
Elimu Taaluma wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Juliana Mlay
(Kushoto) akitafakari nini cha kuwaambia "Wageni" wake, wanafunzi wa
shule za msingi Kijichi na Bwawani za jijini walioandamana umbali wa
kilomita 10 hadi ofisini hapo wakilaani kutosoma jana, kufuatia mgomo wa
walimu ulioanza nchi nzima jana Julai 30, 2012.
Kiongozi
wa wanafunzi walioandamana jana jijini Dar es Salaam, Christofa Msifuni
Msuya wa darasa la saba, shule ya msingi Bwawani, akizungumza kwa niaba
ya wenzake kwenye ofisi za Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke jijini Dar
es Salaam Jumatatu Julai 30, 2012.
Wanafunzi
wa shule za msingi Bwawani na Kijichi, zajijini Dar es Salaam,
wakiamnadmana jana kupinga kile walichokiita kuvurfughwa kwa haki ya
mtoto ya kupata elimu, na hii ni kufuatia mgomno wa walimu ulioanza jana
nchi nzima. Wanafunzi hao waliandamana hadi urefu wa kilomita 10 kutoka
shuleni kwao hadi ofisi ya Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, ziliko
shule hizo, jirani na uwanja wa taifa ili kufikisha kilio chao.
PICHA: Blogu ya Khalfan Hamis
PICHA: Bashir Nkoromo blog
Wanafunzi wakiwa wanaelekea ofisi ya Mkuu wa wilaya
Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.
Moja
ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu hawajaingia
darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake
Wanafanzi
wa darasa la saba shule ya msingi Meta wakiendelea kupeana mazoezi ya
masomo mbalimbali baada ya waalimu wao kugoma kuingia madarasani
Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao
Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma
Picha na Arithy via Mbeya Yetu blog
Mwalimu
wa Shule ya Msingi Mmoja, Salma Mtili akisahihisha daftari la
mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo licha ya rais awa Chama cha
Walimu Tanzaniza (CWT) kutangaza mgomo wa walimu nchi nzima.
Picha na Habari Mseto Blog
Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani katika Manispaa Singida (picha na Nathaniel Limu)
0 comments:
Post a Comment