Boti ya Mv Skagit
Walifikishwa mahakamani saa 3:0 asubuhi akiwemo na Meneja wa Kampuni ya Seagull Sea Transport Limited, Omar Hassan Mkonje (50), ambao ni wamiliki wa boti iliyozama wakiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Walisomewa mashtaka 60 ya uzembe na kusababisha vifo kwa kuzidisha abiria na mizigo na kusababisha kuzama katika eneo la Chumbe Julai 18, mwaka huu.
Mwendesha Mashitaka, Sabra Mselem Khamis, alidai kwamba washitakiwa waliruhusu boti kupakia abiria na mizigo kupita kiwango na kusababisha kuzama.
Alidai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na tuhuma 60 kila mmoja na hawakutakiwa kujibu mashtaka yao.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na Sabra Mselem Khamis na Suleiman Masoud Makame, ulidai kwamba kama Mahakama hiyo ina mamlaka ya kisheria ya kutoa dhamana hawana pingamizi.
Wakili wa utetezi, Abdalla Juma Mohammed, alidai kwamba kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 washitakiwa wanahaki ya kupata dhamana kwa makosa kama hayo.
Alidai kwa mujibu wa katiba makosa yasiokuwa na dhamana ni mashitaka ya uhaini, kupatikana na silaha, kuua kwa kukusudia pamoja na mashitaka ya dawa za kulevya.
Hata hivyo, Mwendesha Mashitaka kutoka Ofisi Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Suleiman Masoud Makame, alidai mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba ni Mahakama Kuu.
Naibu Mrajisi, Ali Ameir Haji, alisema dhamana kwa washitakiwa ipo wazi na kuwataka kutoa fedha tasilimu Sh. milioni tano, na wadhamini wawili kudhamini kiwango cha fedha kama hicho cha maandishi kila mmoja pia wawe watumishi wa Serikali ya Zanzibar.
Hata hivyo, Upande wa utetezi waliomba wayeja wao wapunguziwe masharti ya dhamana badala ya fedha wapeleke nyaraka za mali na kuondoa sharti la wadhamini kuwa lazima wawe watumishi wa SMZ maombi ambayo yalitupiliwa mbali na hakimu.
Wakati huo huo, jana maiti 14 ziliopolewa na kufikisha jumla ya maiti 112 zilizoopolewa.
jamani huyo meneja wa seagull anahusishwaje? na kama anahusika haoni hiro tatizo la hizo meli au anataka kutoa watu kafara? sio vizuri kama mnaona kuna tatizo la kiufundi ni vema yafanyike matengenezo kabla ya madhara maubwa kutokea.
ReplyDeletemeli inazima zaidi ya mara nne baharini lakini mtengenezo ya kina hakuna mpaka itokee ajali badirikeni jamani pesa zina mwisho mkumbuke kuwa uhai haununuliwi muwe mnajali maisha ya watu .
ReplyDelete