Tarehe:7
July,2012:TAMAL HOTEL –MWENGE
AJENDA:
1.Kufungua kikao
2.Utambulisho
3.Jina La kundi
4.Maazimio na Malengo
5.Mengineyo
6.Uchaguzi wa viongozi
MAHUDHULIO:
Waliohudhulia ni jumla ya watu 18.
MAJADILIANO:
1.KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa rasmi saa kumi na
moja na robo (05:15) na kutangulizwa na sala iliyoongozwa na Mr.Rugalabamu
2.UTAMBULISHO
Mwenyekiti wa mda Mr Nelson Bagenda
aliomba kila mjumbe kujitambulisha kwa majina kamili,mwaka aliomaliza Dsm
Secondary,na Historia yake fupi baada ya hapo mpaka sasa.kila mjumbe alifanya
hivyo na kupongezana.
3.JINA LA KUNDI
Wajumbe walipendekeza Majina Kadhaa la kundi kama.Lenga
Mbali Daima,x-Dar Seco ,DARSEU nk.na jina lililopitishwa ni DARSEU kifupi cha neno Dar es salaam Secondary Unity.
4.MAAZIMIO NA MALENGO
Ilishauliwa kua DARSEU ilenge
kumsaidia mwanachama wake katika SHIDA na RAHA
SHIDA:Msiba(Mume,Mke,Mtoto,Mama na
Baba Mzazi).Ugonjwa kwa mwanachama,na Majanga (Moto na,Mafuriko)
RAHA:Harusi na Uzazi.
5.MENGINEYO
(i)
IDADI YA WANACHAMA:
Imeshauliwa kuwe na Limit (Idadi
kamili) ya wanachama ilikuwe na uwezo wa kujiongoza kuliko kuwa watu wengi
zaidi.Na iliafikiwa DARSEU isizidi zaidi ya wanachama Hamsini(50) pekee.
(ii)JINSI YA KUPATA MAPATO
Wajumbe walipendekeza kuwe na Michango ya kila Mwezi pia na Ada ya
kiingilio kwenye Kundi.
Makubaliano ada ya Mwezi. TZS 5,000/=,Ada ya Kiingilio(usajili) TZS 5,000/=
(kwa walio hudhuria kikao) .Atakaejiunga baada ya hapo ni TZS 10000/=.
Wajumbe wote 18 walitoa TZS 5,000/= (ada ya usajili) jumla TZS 90,000/=na
pia uchakavu wa TZS 5,000/= (Iliotumika kwenye vinywaji na kulipia eneo la
kikao TAMAL HOTEL ) Jumla 90,000/= Vinywaji TZS 72,500/= Eneo TZS 20,000/=
(iii)Ilishauliwa pia kuwe na kiwango
cha vinywaji kwenye vikao vya chama Mf.Bia mbili walau ilikumbunguza gharama
zisizo na msingi.Alkadhalika wajumbe walishauli vikao view vinatembea (Rotate)
kulingana na Makazi ya wanachama.isiwe sehem moja pekee.
6:UCHAGUZI WA VIONGOZI
Mr .Godfrey Rugalabamu .Mwenyekiti alipendekezwa na kupitishwa.
Mr.Pasco Athanas
Katibu alipendekezwa na kupitishwa
Miss.Happy Minja
Mweka Hazina nae alipendekezwa na kupitishwa
Mwenyekiti (Godfrey)alihairisha kikao
saa Moja na nusu (07:30) mpaka hapo itakapo tangazwa..
0 comments:
Post a Comment