Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6
mwaka huu) na shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa
(Taifa Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba
145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.
Mei 26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi
na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano
kutoka ya 102 hadi 107.
Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu
iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15
hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande
wan chi za Afrika katika viwango hivyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment