Afisa mkuu anayehusika na
masuala ya watoto na mizozo, Radhika Coomaraswamy, ameiambia BBC kuwa
hajawahi kushuhudia hali kama hiyo ambapo watoto hawahurumiwi na
kulengwa kwenye mashambulio.
Akizungumza kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Coomeraswamy ameiambia BBC kuwa ni jambo la kawaida kuwaona watoto wakiuawa au kujeruhiwa wakati wa vita, lakini ameongezea kuwa ni jambo la kusikitisha kuona watoto wanateswa na kudhulumiwa wakiwa kizuizini au hata kuuawa kinyama, kama vile wanavyotendewa nchihi Syria na wanajeshi wa serikali.
Pia
amewashutumu wapiganaji wa upinzani wa Free Syrian Army kwa kuwatumia
watoto chini ya umri wa miaka kumi na sita katika mstari wa mbele wa
mapigano.
Coomeraswamy amesema watoto kadha wamejitokeza
na kudai kuwa walitekwa nyara na kulazimishwa kuabiri magari ya kivita
na kutumiwa kama ngao na wanajeshi wa nchi hiyo.
Ameongeza kuwa makundi kadhaa ya waasi pia
yamewasajili watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi na sita kuwa
wanajeshi wao. Wengi wao wanatumiwa kama wahudumu wa afya na pia kama
mabawabu mbali na kuwekwa katika mstari wa mbele wa vita.
Bi Coomeraswamy sasa amejumuisha wanajeshi wa
Syria katika orodha ya Umoja wa Mataifa ya mataifa yanayowadhulumu na
kuwauawa watoto, kushambulia shule na hospitali mbali na kuhusika na
visa vingine vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Mataifa mengine ambayo yamewekwa kwenye orodha hiyo afghanistan na Iraq pia yamejumuishwa kwenye orodha hiyo ya aibu.
Amesema mzozo wa kisiasa nchini syria umepoteza
mwelekeo na kuwa wanajeshi wa serikali na waasi hawatofautishi raia na
maadui wao na hivyo wanachukua maamuzi ya pamoja ambayo watoto
wanalengwa
0 comments:
Post a Comment