Wauguzi
na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakilisukuma gari
la wagonjwa lililombeba mpigania haki zao Dk. Ulimboka wakati
akitolewa chumba cha X-ray akipelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI).
Madaktari wakisaidia kumuingiza Dk.Ulimboka katika gari la wagonjwa namba T 151 AVD la Hospitali ya AAR.
|
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akitoa taarifa ya kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoratibu mgomo wa madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, Dar es Salaam jana. |
Dk.
Cathbert Mchalo wa Taasisi ya Mifupa ya Moi (kushoto), akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kumpokea, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari Tanzania kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha
aliyopata kutokana na kipigo.
Ofisa
wa Polisi akimzuia mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Francis
Dande, asimpige picha wakati wakimuondoa askari mwenzao
aliyeshambuliwa na madaktari akituhumiwa kukutwa akipiga simu ya
kuwataarifu wenzake kuwa Dk. Ulimboka hakufa.
Mmoja
wa wana usalama wa (wa pili ushoto), akizozana na madaktari baada ya
kumbaini akijifanya ni mwandishi wa habari na kumuamuru kuondoka
eneo hilo mara moja.
Mmoja
wa madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wa pili
kulia, akizozana na Askari Polisi waliofika hospitalini hapo wakidai
wanatafuta redio yao ya mawasiliano iliyopotea wakati wa pilikapilika
za kumpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa
madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, alipoletwa akiwa hoi kutokana
na kipigo kutoka kwa watu waliomteka usiku wa kuamkia jana na kumtupa
msitu wa Mabwepande.
Madaktari wakiwa wamepigwa butwaa nje ya viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia tukio hilo.
|
Wauguzi wakiwa nje ya wodi ya Kibasila wakitafakari jambo kufuatia jambo hilo
0 comments:
Post a Comment