Mgonjwa
akihamishwa kutoka Wodi ya Kibasila katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), iliyopo Dar es Salaam jana, ili kupelekwa katika
hospitali nyinyine kutokana na tihsio la kuwepo kwa mgomo wa madaktari,
katika hospitali hiyo na nyingine za serikali sehemu mbali mbali
nchini wanaodai stahiki zao mbali mbali, kwa madai ya serikali
kushindwa kuzitekeleza
MADAKTARI
nchini wameanza mgomo katika baadhi ya hospitali nchini baada ya
Serikali kushindwa kutekeleza madai yao waliyowasilisha katika Kamati
ya Majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Mgomo huo
umetangazwa na Jumuiya ya Madaktari nchini huku ikifafanua kwamba kati
ya madai kumi waliyotaka yatekelezwe na Serikali, hakuna hata moja
lililofanyiwa kazi.
Hata
hivyo, jana madaktari hao ambao walikaa vikao vya majadiliano na
Serikali kwa siku 90 baada ya kusitisha mgomo wao wa pili, wamesema
katika madai yao kumi, hakuna hata moja lililotekelezwa na Serikali.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Stephen Ulimboka jana aliwaeleza
waandishi wa habari kwamba ili warejee kazini, Serikali inatakiwa
kutekeleza madai yao yote na kusisitiza kwamba dai lao la kwanza ni
kuitaka Serikali kuboresha huduma za msingi kwa wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment