Downing amesema kikosi cha England kamwe hakitababaika wakati watakapokutana na Ufaransa siku ya Jumatatu.
Meneja
Roy Hodgson ataiongoza England katika mechi yao ya kwanza dhidi ya
Ufaransa, kabla ya kucheza na Sweden tarehe 15 Juni, na siku nne
baadaye, kupambana na wenyeji Ukraine.
Downing, mwenye umri wa miaka 27, amesema: "Tuna imani kwamba tutapata matokeo mazuri. Hatuwaogopi."
"Tunajua timu yao ni nzuri, lakini hata sisi hucheza vizuri. Tunazifahamu nguvu zao na vile vile udhaifu."
Alikanusha kwamba wachezaji wa England wamekuwa
wakizungumza kuhusu mchezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand, kwa
kuachwa nje ya kikosi hicho.
"Yeyote meneja atakayemchagua tunaweza kuendelea
naye. Mimi najitahidi zaidi kuangazia nafasi ninayocheza, na wenzangu
katika timu wanafanya vivyo hivyo."
Downing ni kati ya wachezaji sita wa klabu ya Liverpool katika timu ya taifa ya England.
Timu hiyo ina wachezaji wengi zaidi katika timu
ya taifa kuishinda klabu yoyote nchini England, licha ya klabu kumaliza
katika nafasi ya nane katika ligi kuu ya Premier.
Downing, ambay zamani aliichezea Middlesbrough
na Aston Villa kama kiungo wa kati, aliitetea klabu yake ya Liverpool:
"Ikiwa utaangalia namna tulivyocheza, tuliweza kuzishinda vibaya timu
wakati mwingine, lakini tulishindwa kupata nguvu katika kumalizia ligi."
0 comments:
Post a Comment