Na Ayoub Mangi
Staa mwenye jina kubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuchangia ‘malavidavi’ na mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ juzikati aliwaacha watu midomo wazi kufuatia kutinga na mbwa wake kwa fundi cherehani kwa ajili ya kumpima nguo.

Kituko
hicho kilishuhudiwa na mwandishi wetu na wapita njia wengine ambapo
staa huyo alitinga kwa fundi maeneo ya Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwa
ajili ya kumshonea nguo za ‘kisista duu’ mbwa wake ‘aliyembatiza’ jina
la Fiona.
Mbele
ya fundi, Wema alitoa maelekezo kwamba anataka Fiona ashonewe nguo za
rangi mbalimbali ambazo yeye anazo ili wakitoka wote wawe wanamechisha.
“Sikia fundi, nataka umshonee nguo za kisista duu za rangi mbalimbali, siku nikitoka naye ‘out’ tunavaa sare, sawa ee?” Alisikika akisema Wema.
“Sikia fundi, nataka umshonee nguo za kisista duu za rangi mbalimbali, siku nikitoka naye ‘out’ tunavaa sare, sawa ee?” Alisikika akisema Wema.
Hata
hivyo, baadhi ya watu walikichukulia kitendo hicho kama kufuru kwa
Mungu wakidai kuwa kuna binadamu wana shida ya mavazi, hivyo ni vyema
kama mlimbwende huyo angewasaidia wahitaji hao kuliko mbwa ambaye
alivyoumbwa Mungu alimfanya asiwe anavaa nguo.
Baada
ya kumaliza ratiba yake kwa fundi, mnyange huyo alielekea duka la
vipodozi kwa lengo la kununua vibanio vya vywele kwa ajili ya Fiona
ambaye ana manyoya mengi kwenye paji la uso.
“Unajua
mbwa wangu huyu ana manyoya mengi kwenye paji la uso, hivyo nakwenda
dukani kumnunulia vibanio vya kubana ili asipate tabu kuona,” alisema
Wema.
0 comments:
Post a Comment