Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.
Uchunguzi
unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za
mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu.
Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya
mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume
ambaye anatajwa kuwa na uwezo kuficha mawazo yake.
Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.
Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.
Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.
KUPENDA KUJITENGA
Mwanamke
ambaye anapenda kujitenga na mpenzi wake atakuwa kwenye hatua za awali
za kuelekea kuachana naye. Tabia ya mwanamke kutopenda kukaa karibu na
mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara ya kuchoka au kukinai
penzi. Hoja inabaki pale niliposema pa yeye kushindwa kuamua haraka na
hivyo kutengeneza kwanza hali ya kumpuuza mpenzi wake.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Mwanamke
ambaye hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi wake yuko kwenye
hatua za kuacha. Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria utoshelevu wa
kihisia ambao ndiyo unaoelezwa kuwa ni muhimu kwenye uhusiano wa
kimapenzi kuliko kitu kingine chochote.
Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.
Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.
KUPENDA KUKOSOA
Kama
nilivyosema, kujua historia ya penzi lenu namna lilivyoanza ni jambo
muhimu kwa sababu husaidia kujua kama kuna mabadiliko hatari ya tabia za
mwanamke.
Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.
Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.
UHUSIANO NA MTU MWINGINE
Licha
ya kwamba usaliti kwenye uhusiano limekuwa suala la kawaida siku hizi,
lakini mwanamke ambaye atakuwa hafichi uhusiano wake wa pembeni na
kuacha minong’ono ikikufikia huku yeye akionesha kutojali malalamiko
yako ya kusalitiwa, ujue hiyo ni ishara kwamba mwanaume wa pembeni
amemfikisha kwenye hitaji la moyo wake na hivyo kuachana na wewe si
jambo la gharama kwake.
KUTOKUKUTEGEMEA
Mwanamke
ambaye ana kusudio la kukuacha huanza kwa kuuondoa utegemezi. Ikiwa
alikuwa anakuomba nauli, fedha ya matumizi, ada na huduma nyingine
atasitisha bila kukuambia na bado utaona anaendelea kujimudu kama
kawaida au kuteseka kimya kimya. Kuacha kukutegemea kama zamani ni
dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri uwezekano wa
kukuacha wakati wowote.
0 comments:
Post a Comment