Tangazo la matokeo ya uchaguzi
wa urais uliofanyika mwishoni mwa wiki limehairishwa, hii ni kulingana
na taarifa kwenye televisheni ya kitaifa.
Matokeo hayo yalikuwa yatangazwe alhamisi,
lakini tume ya uchaguzi imelazimika kuhairisha tangazo hilo ili
kushughulikia malalamiko yaliowasilishwa na wagombea.Msemaji wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, Nader Omran amesema kuwa tangazo hilo halifai kuhairishwa.
"Hatua hii itachochea hali ya wasiwasi itakuwa bora zaidi suala hili limalizwe alhamisi" amesema Bw Omran.
Wasimamizi wa kampeni ya mgombea wa Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi wanasema kuwa kura zinaonyesha kuwa alishinda duru hiyo ya pili ya uchaguzi.
Lakini mshauri wa karibu wa Ahmed Shafiq, amewaelezea waandishi wa habari mjini Cairo kuwa, Shafiq- aliyekuwa waziri mkuu chini ya Utawala wa rais Hosni Mubarak-alishinda uchaguzi huo.
Maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani ya Tahriri tangu juzi kulaani baraza kuu la jeshi ambalo juzi limejilimbikizia mamlaka baada ya mahakama kuu kulivunja bunge la nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment