SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la PEN-TRUST lenye makao yake
makuu katika mji wa Minesota nchini Marekani linatarajia kutoa msaada wa
umeme wa nishati ya jua katika shule za sekondari za kata kumi mkoani
Singida.
Mwenyekiti wa shirika hilo nchini, Athumani Mungwe alisema shule hizo
kumi zitakazopokea msaada huo ni kati ya sekondari 156 zilizopo mkoani
hapa.
Alizitaja shule zitakazonufaika na mradi huo kwa awamu ya kwanza kuwa ni Ikhanoda, Mwasauya, Mughamu, Itaja na Maghojoa.
Nyingine ni Mikiwu, Madasenga, Makuro, Matumbo na Merya.
Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone licha
ya kukiri kupokea misaada mingi kutoka kwenye shirika hilo, hakusita
kuwasilisha ombi jingine la vitabu kwa ajili ya shule za msingi zilizopo
mkoani hapa.
Hata hivyo, Dk. Kone alifafanua kwamba alishiriki katika kutoa wazo la
shirika hilo kuweka nishati ya umeme wa jua katika shule za sekondari
kwa kupendekeza kuanzishwa kwa maktaba katika shule za sekondari na
kuweka huduma hiyo ya umeme wa sola.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa huyo hakusita kusisitiza umuhimu wa
kuwakumbuka watu wenye ulemavu kwa madai kwamba ni kundi ambalo bado
linahitaji kukumbukwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na makundi mengine
ya jamii.
0 comments:
Post a Comment