Askari Magereza wakilinda basi alilopakiwa Lulu.
Basi alilopakiwa Lulu likiingia mahakamani.
Lulu akishuka.
…Akisubiri kusomewa kesi yake.
Ulinzi mkali nje ya mahakama.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
leo imempa ushindi msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael
‘Lulu’, katika kesi ya kujadili upya umri wake. Akitangaza ushindi huo
jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Twalib Fauz, ameupa ushindi upande
wa utetezi uliopeleka ombi la kuujadili upya umri wa msanii huyo na
kuutupilia mbali umri wa miaka 18 alioandikisha kituo cha polisi baada
ya kukamatwa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)
0 comments:
Post a Comment