Hii
ndio Hali hali halisi katika Hospitali ya Mkoa Mbeya, huku wakina mama
wajawazito wakiwa wamelala wawili mpaka wa tatu katika Kitanda kimoja.
Wakina
mama hao ambao wengi wao wamekimbia katika Hospitali ya Wazazi Meta
baada ya kukosa huduma ya matibabu ya uzazi kutokana na mgomo wa
Madactari unao endelea Nchi nzima
Baadhi ya kina mama wajawazito wakiwa katika foleni ya kungoja kumuona Dactari
Mama
Sophia Mwangwata kutoka Tunduma akiwa amemleta mwanae kuja kujifungua
katika hospitali ya mkoa Mbeya , baada ya kukosa huduma huko Tunduma.
Wakina
mama walio jifungua salama wamemshukuru sana mganga wa hospitali hiyo
,kwa huduma waliyo pata kujufungua salama, huku wengine wakisema
Madactari walio goma hawana wazazi wala watoto wanao umwa
Hiki
ndicho chumba kikuu cha upasuaji, Madactari walio kuwepo eneo hilo
wamegoma kutokeza kwenye Kamera ya Mbeya yetu lakini wamedai kuwa , kila
siku zaidi ya wanawake 15 hujifungua kwa njia ya upasuaji,hivyo kufanya
kazi hiyo ya upasuaji kuwa ngumu sana na kuwaomba madactari wenzao
warejee kazini ili waweze kusaidiana kazi hiyo,kwani wagonjwa ni
tofauti na Chuma au Gari hawana Spea, Tofauti na magari unaweza ngoja
spea ndio ukarekebisha lakini kwa Binadamu ukingoja atakufa.
Mama akiwa amelala Chini ya Godoro pamoja na kachanga kaliko zaliwa muda si mrefu uliopita
Umati wa wagonjwa unazidi kuongezeka katika Hospitali hiyo ya mkoa Mbeya
0 comments:
Post a Comment