Bao la Ricardo Vaz Te katika dakika za majeruhi liliapatia klabu ya West Ham ushindi na tikiti ya kurejea katika Ligi kuu ya Premiership baada ya msimu mmoja katika daraja la championship.
Pande zote mbili zilikua na kosa kosa nyingi ingawa ni timu kutoka London iliyotumia fursa muhimu ambapo mshambuliaji Vaz Te aliyesajiliwa hivi katika dirisha la mwezi Januari kutoka klabu ya Barnsley, kujikuta peke yake na kupiga mpira kutoka umbali wa yadi 12 kuwainua mashabiki wa Hammers.
Bao hili pia lina maana kua West Ham imeweza kushinda mechi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa
Wembley katika kipindi cha miaka 31, na kurejea kwake baada ya kushuka daraja kwa kipindi cha mwaka mmoja wanafuata rekodi ya mwaka 1996 ya klabu ya Leicester.
Furaha ya West Ham hata hivyo, yaligeuka kua majonzi kwa Blackpool iliyoshuka daraja pamoja na West
Ham msimu uliopita haikujaliwa kurejea katika Ligi kuu.
Msisimko ulijitokeza wakati mmoja ikionekana kama Blackpool inaweza kurudisha bao na kusababisha mda wa ziada wa kuamua mshindi lakini kujeruhiwa kwa mshambuliaji Gary Taylor Fletcher kulipunguza matumaini na kuiongezea West Ham matumaini.
0 comments:
Post a Comment