Shirika la kuteteta maslahi ya
watoto la The African Child Policy Forum linasema zaidi ya watoto elfu
40 wameasiliwa katika kipindi cha miaka minane wengi wakiwa na walezi
kutoka Marekani, Ulaya Magharibi na Canada. Watoto wengi hasa
wanaasiliwa kutoka Ethiopia ambayo inatuma watoto wengi ugenini nyuma ya
China.
Kuna zaidi ya mashirika 70 yanayoshughulika na
mpango wa kuwaasili watoto nchini Ethiopia 15 ya mashirika yakiwa ni ya
Kimarekani.
Sababu kubwa ya barani Afrika kuwa na idadi
kubwa ya watoto wanaoasiliwa na wageni ni kutokana na udhibiti mkubwa wa
mpango huu katika mataifa ya Ulaya na Amerika Kusini.
The African Child Policy Forum inasisitiza haja
ya kila mtoto kukulia katika mazingira yake asilia ya kuzaliwa. Shirika
hili linasema ni muhimu kwa mtoto kukua na jamaa na utamaduni anaofahamu
zaidi.
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment