WATU wanne wametiwa mbaroni na jeshi la polisi katika ‘njia ya panya’
mpakani mwa Tanzania na Kenya, mkoani Arusha baada ya kukutwa na magunia
50 ya bangi yenye thamani ya mamilioni ya fedha wakiwa njiani kupelekwa
Kenya.
Waliokamatwa ni pamoja na wakulima Babuu Laizer (34) na Lomnyaki
Lekibengi (30), dereva wa lori dogo aina ya Toyota DCM lenye namba za
usajili T922 AFJ lililokamatwa likiwa na mzigo huo, Edward Mollel na
utingo wake, John Joshua (36).
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Thobias Adengenye alisema
watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa 9 alasiri katika kijiji
cha Sinya Vilima Saba mpakani mwa Kenya na Tanzania katika njia za
panya.
Andengenye alisema polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori
walifanikiwa kukamata watu hao wakiwa na mifuko 50 ikiwa na bangi ndani
gari hilo mali ya Zephania Kambei mkazi wa Ngaramtoni mkoani Arusha.
Alisema dawa hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka vijiji vilivyo
kando kando ya mlima Meru kuelekea Nairobi nchini Kenya kupitia njia
isiyo rasmi maarufu kwa `njia ya panya’ iliyopo huko Sinya vilima saba.
Home
»
»Unlabelled
» Wanaswa Arusha na lori lenye magunia 50 ya bangi
Saturday, May 26, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment