Friday, May 18, 2012

   
Tamko la Chadema
Katibu wa Chadema Manispaa ya Iringa akitoa tamko kuhusu shambulio kwenye mkutano wao wa hadhara uliofanyika tarehe 13/05/2012 katika Kata ya Nduli na kusababisha Vijana wanne kuumizwa na mapanga kati yao wawili kuwa katika hali mbaya na iliyopelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa  Iringa. Pamoja na Mbunge la Jimbo la Iringa Mchg. Peter Msigwa kutishiwa kuuawa.

Shambulio hilo lilifanywa na Vijana wa familia ya Ndugu Idd Chonanga ambaye ni Mheshiwa Diwani wa Kata ya Nduli (CCM).
Kwa bahati mbaya  mpaka sasa hakuna uongozi wa Serikali au Kiongozi yoyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa ambaye   ameonyesha kulaani vitendo hivyo vya kikatili. Hata hivyo tunatoa shukrani kwa Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa vurugu hizo. Aliongeza kwa kusema hakuna lolote la kuzungumza kama Chama kwa sababu tunasubiri maamuzi ya Mahakama.  Pia aliongeza kuwa kuna mtuhumiwa mmoja (Hamis Chonanga) anatakiwa akamatwe kwa kuwa na yeye ni miongoni mwa washtakiwa wanne walikwishafikishwa mahakamani.

Mheshimiwa Mbunge aliwatahadharisha wanachama na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi hiki.

POLISI WASITISHA MIKUTANO YA CHADEMA
Polisi Mkoa wa Iringa wamesitisha kufanyika kwa mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  baada ya Chadema kuomba kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa. Wakirudishiwa  majibu ya barua yenye Kumb. Na. IRIA.23/14/VOL. XII/213 ya tarehe 16/05/2012 inasema“YAH: KUSITISHA MKUTANO WA HADHARA KATIKA VIWANJA VYA MWEMBETOGWA TAREHE 18/05/2012. Tafadhari rejea barua yako yenye Kumb. na. CDM/IR/M/20/012 ya tarehe 15/05/2012. Kutokana na hali ya utulivu kutokuridhisha mikutano yote imesitishwa hadi hapo kutakapotokea hali ya utulivu.” Ilisomeka barua hiyo.

0 comments:

Post a Comment