Msanii nyota wa filamu anayesumbuliwa na uvimbe tumboni, Juma Kilowoko `Sajuki'`
Safari
ya msanii nyota wa filamu anayesumbuliwa na uvimbe tumboni, Juma
Kilowoko 'Sajuki' ya kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu imeiva,
baada ya wasamaria wema kumchangia kiasi cha Sh. milioni 16.
Japo
fedha hizo ni pungufu ya Sh. milioni 9 ya fedha zote zilizokuwa
zikihitajika kwa ajili ya safari ya msanii huyo kwenda nchini humo
kutibiwa, lakini mkewe Wastara Juma ameshukuru kwa sababu inamwezesha
mumewe kusafiri.
Akihojiwa
na kituo kimoja cha redio, Wastara, alisema anawashukuru watu wote
waliofanikisha kupatikana kwa fedha hizo pamoja na tiketi tatu za ndege
za kumsafirisha mgonjwa, yeye na kaka wa Sajuki kwenye matibabu hayo.
"Kwa
kweli nawashukuru watu wote waliojitolea kwa hali na mali kumsaidia
mume wangu kwani nimefanikiwa kupata Sh. milioni 16 kati ya Sh. milioni
25 zilizokuwa zikihitajika," alisema.
Aliongeza
kutokana na kupatikana kwa fedha hizo huenda wakaondoka nchini kwenda
India kwenye matibabu kati ya Jumapili au Jumatatu ijayo.
"Nadhani
kati ya Jumatatu au Jumapili ijayo tunaweza kusafiri ambapo mbali na
Sajuki mwenyewe, kwenye msafara nitakuwepo na mimi na kaka wa Sajuki,"
alisema.
Hata
hivyo Wastara alinukuliwa akilia na watu waliomliza kiasi cha Sh.
800,000 katika akaunti yake ya simu iliyokuwa ikitumiwa kuchangishia
fedha hizo, ingawa anaendelea kuzifuatilia katika makao makuu ya mtandao
huo wa simu za mikononi.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment