Chama tawala nchini Afrika
Kusini ANC, kimesema kinachukua hatua za kisheria kulazimisha nyumba
moja ya sanaa ambayo inaonyesha picha ya rais Jaocob Zuma, sehemu zake
za siri zikiwa nje kuondoa mchoro huo.
Msemaji wa chama ametaja picha hiyo kama inayoudhi, ya kuchukiza na yenye matusi.
Mchoro huo ni sehemu ya maonyesho ya michoro
mjini Johannesburg yenye kauli mbiu ' Sifa kwa mwizi' na ambayo
inajumuisha michoro yenye lengo la kukosoa chama tawala ANC.
Mchoraji wa picha hiyo Brett Murray, alisema kuwa picha zake zenyewe zinajieleza.
CHANZO BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment