Tuesday, May 15, 2012

HABARI hii haina lengo la kumhukumu mtu, mwenye uwezo huo ni Mwenyezi Mungu pekee, lakini Ijumaa Wikienda lina orodha ndefu ya warembo waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ ambapo uchunguzi umethibitisha kuwa, kifo cha staa huyo kimewaacha ‘wajane’ hao katika vilio vya kila kukicha.
Uchunguzi makini uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa nyota huyo alikuwa na uhusiano na wasichana mbalimbali wakiwemo ma-miss, wanamuziki, wasanii wa sinema na wasio na fani yoyote ile.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kifo cha Kanumba bado kinawachuruzisha machozi wasichana hao kama inavyokuwa kwa wanawake walioolewa halafu wakaondokewa na waume zao (wajane).
‘Wajane’ hao waliotajwa kuendelea kumwaga machozi ni kama ifuatavyo;
WEMA SEPETU
Ni Mrembo wa Tanzania mwaka 2006/07 ambaye kwa sasa ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo. Awali yeye na marehemu Kanumba walijaribu kuficha penzi lao lakini kadiri siku zilivyosonga, hakukuwa na kificho tena.
Kifo cha Kanumba ni pigo kwake, bado anamlilia hadi sasa. Wakati wa msiba alikiri kuwa hakuwahi kutengana moja kwa moja na marehemu.
SYLVIA SHALLY
Ni mrembo wa Miss Dar City Centre 2009, alikuwa na uhusiano na Kanumba, walianza walipokutana katika shindano la kumtafuta Unique Model kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar.
Yeye bado hajaamini kama staa huyo aliaga dunia ghafla.
QUEEN SUZY
Ni Mnenguaji wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano na marehemu Kanumba wakati fulani akipiga mzigo kwenye Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambapo mara nyingi Kanumba alikuwa akienda nyumbani kwake.
Anasema kifo cha Kanumba mpaka sasa bado ni ndoto kwake na hakuamini.
SHAMSA FORD
Orodha inamtaja mcheza filamu huyu ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na marehemu wakati wakiigiza sinema ya Saturday Morning.
Kifo cha Kanumba kwake ni pengo kwa sababu ndiye aliyemwingiza kwenye ‘gemu’ la sanaa ya maigizo na atamlilia marehemu kila atakapokuwa akimkumbuka.
AGNESS GERALD ‘MASOGANGE’
Orodha hiyo inamjumuisha muuza nyago huyu kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva na filamu ambaye anadaiwa aliwahi kuwa na uhusiano na Kanumba wakiwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar.
Kifo cha Kanumba anasema bado kinamchuruzisha machozi kila anapokumbuka, hasa mara ya kwanza alipopokea taarifa za kufariki kwake.
SHARZ
Huyu ni mrembo aliyecheza filamu ya marehemu iitwayo The Shock. Ndiye mpenzi wa Kanumba aliyetangaziwa kuolewa, lakini ghafla waliachana na Sharz hajaonekana tena kwenye muvi.
Kifo cha marehemu kilimkuta akiwa masomoni, Kenya. Kilio chake anasema kitadumu na kudumu na kudumu.

AUNT EZEKIEL
Ishu ilibumburuka mwaka jana pale Klabu ya Bongo Movie (Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar) ilipotangaza kumsimamisha ndipo yakaibuka makubwa kuwa alifanyiwa hivyo kwa sababu alimmwaga Kanumba. Baada ya hapo uhusiano wao ukakatika.
Alikuwa mstari wa mbele kwenye kifo cha marehemu, mpaka Muhimbili kuuhifadhi mwili. Anasema hatakaa asahau kifo hicho.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Kwa sasa anashikiliwa na sheria kwenye Gereza la Segerea, Dar akiwa mshukiwa wa kwanza katika kifo cha Kanumba kufuatia ugomvi wa kimapenzi kati yao.
Siku ya tukio, baada ya ugomvi huo Lulu aliondoka na huko alikokwenda alipata habari kwamba mpenzi wake huyo amefariki dunia, akasema haitatokea akaamini.
SALMA HAMIDU
Ni mdada mkazi wa jijini Mwanza, yeye anatajwa kwenye listi ya ‘wajane’ kufuatia hivi karibuni kuibuka akidai ana mtoto wa kike aliyezaa na marehemu Kanumba aitwaye, Treasure.
Kwa vyovyote vile, kwa kuondokewa na mzazi mwenzake, Salma atakuwa analia kila kukicha, hasa anapomwangalia Treasure.
PASCALIA MACHA
Ni mkazi wa Sumbawanga, Rukwa. Aliibuka na kudai akiwa anaishi Dar, aliwahi kuwa na uhusiano na marehemu na kufanikiwa kupata naye mtoto.
ISABELLA FRANCIS
Huyu ni msanii anayekuja juu kwenye tasnia ya uigizaji Bongo. Amewahi kukiri kuwa ‘alishatoka’ na marehemu kwa mapenzi motomoto na wakamwagana bila bifu.
Kifo cha mpenzi wake huyo kwake ni kitendawili ambacho anaamini siku si nyingi, Mungu atakitegua kuwa maigizo na uhalisia wa marehemu utarudia kama zamani.
WALIOKWENDA NYUMBANI KWA MAMA KANUMBA
Wajane hao hawajaishia hapo kwani wiki mbili baada ya kifo cha staa huyo wa filamu za Bongo wako warembo, kwa nyakati tofauti, waliokwenda nyumbani kwa marehemu maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza na kumkabili mama’ke wakimwambia wao walikuwa wachumba wa Kanumba.
Mama Kanumba aitwaye Flora Mtegoa aliwahi kukiri kwa mapaparazi kuhusu ‘wachumba’ hao ambapo alisema idadi yao ilifikia watano.
TUNAMNUKUU:
“Sishangai kusikia kuna wanawake wanaodai walizaa na marehemu mwanangu maana hapa wameshakuja wasichana, nadhani wamefika watano sasa, kila mmoja anadai yeye alikuwa mchumba wa marehemu (kicheko cha uchungu).” CHANZO CHA HABARI GLOBAL PUBLISHERS

0 comments:

Post a Comment