Thursday, May 24, 2012



Na Shakoor Jongo
MWIGIZAJI wa ‘long time’ katika sinema za Bongo, Tamlina Mohamed Poshi ‘Amanda’ (pichani) anadaiwa kukimbiwa na mumewe, Khamis Bwela .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri baada ya Amanda kwenda kwao Mbezi, Dar kwa ajili ya kuuguza mguu ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
“Unajua Bwela alikuwa tayari kishamchoka mkewe kutokama na mambo f’lanif’lani akawa anajiandaa kumtoka kwa siri kwenda nchini Japan kuishi kwa muda mrefu.
“Kwa hiyo kitendo cha Amanda kwenda kuuguza mguu kwao, mwenzake alipata nafasi, alikata tiketi akakwea pipa na kutimkia huko huku akikabidhi vitu vyake kwa ndugu,” kilidai chanzo hicho.
Ikadaiwa kuwa, Amanda aliporudi nyumbani alishangaa kukuta hakuna dalili ya kuwepo kwa mtu kwa siku mbili tatu nyuma, majirani wakamtonya kuwa mumewe alionekana akihamisha vitu.
Baada ya kupata taarifa hizo, paparazi wetu alimvutia ‘waya’ Amanda ili kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka hivi:
“Huyo aliyekupa taarifa hizo amekosea, kwani ningeagwa na nisingeangwa yote ni sawa tu kwa vile huyo mtu mimi siko naye.”

CHANZO GAZETI LA AMANI LA LEO

0 comments:

Post a Comment